Ubaguzi wa rangi lingali tatizo kubwa katika jamii ya Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i45200-ubaguzi_wa_rangi_lingali_tatizo_kubwa_katika_jamii_ya_marekani
Matokeo ya uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa nchini Marekani yanaonyesha kuwa Wamarekani wengi wanaamini kwamba ubaguzi wa rangi lingali ni tatizo kubwa na muhimu katika jamii yao.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 30, 2018 23:10 UTC
  • Ubaguzi wa rangi lingali tatizo kubwa katika jamii ya Marekani

Matokeo ya uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa nchini Marekani yanaonyesha kuwa Wamarekani wengi wanaamini kwamba ubaguzi wa rangi lingali ni tatizo kubwa na muhimu katika jamii yao.

Gazeti la The Independent limeandika kuwa karibu theluthi mbili ya watu waliotoa maoni yao kwenye uchunguzi uliofanywa na kanali ya uchunguzi wa maoni ya NBC News-SurveyMonkey wamesema ubaguzi wa rangi ungali ni tatizo muhimu katika jamii ya Marekani, huku robo tatu ya walioshiriki kwenye uchunguzi huo wa maoni wakisisitiza kuwa ubaguzi dhidi ya Wamarekani wenye asili ya Afrika ni tatizo kubwa sana.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, wakati asilimia 30 ya Wamarekani wanahisi ubaguzi wa rangi si suala muhimu, watu haohao wanakiri kuwa suala hilo lipo katika jamii ya Marekani huku majibu mengine ya uchunguzi huo wa maoni yakionyesha kuwa Wamarekani wanatafautiana sana kuhusu nafasi ya asili na rangi ya mtu katika jamii ya nchi hiyo.

Gazeti la The Independent limemalizia kwa kukumbusha kuwa asilimia 57 ya watu waliotoa maoni yao wanaamini kwamba ndani ya jamii ya Marekani, raia wazungu wanapewa upendeleo mkubwa zaidi kuliko wenzao wenye asili ya Afrika.../