Wajerumani waandamana wakiitaka Marekani kuondoa silaha zake za nyuklia nchini mwao
https://parstoday.ir/sw/news/world-i46036-wajerumani_waandamana_wakiitaka_marekani_kuondoa_silaha_zake_za_nyuklia_nchini_mwao
Taasisi za Ujerumani zinazounga mkono amani zimeitisha maandamano makubwa ya amani yenye lengo la kuishinikiza Marekani kuondoa silaha zake za nyuklia zilizopo nchini mwao.
(last modified 2026-05-20T03:07:53+00:00 )
Jun 18, 2018 21:52 UTC
  • Wajerumani waandamana wakiitaka Marekani kuondoa silaha zake za nyuklia nchini mwao

Taasisi za Ujerumani zinazounga mkono amani zimeitisha maandamano makubwa ya amani yenye lengo la kuishinikiza Marekani kuondoa silaha zake za nyuklia zilizopo nchini mwao.

Gazeti la Süddeutsche Zeitung la Ujerumani limeandika kuwa taasisi hizo zinalalamikia uwepo wa silaha za maangamizi za Marekani katika kambi ya kijeshi ya anga iliyopo jimbo la Rhineland-Palatinate nchini Ujerumani. Limefafanua kuwa washiriki wa maandamano hayo yaliyofanyika juzi Jumapili, wamesisitizia udharura wa kuondolewa kwa silaha hizo za Marekani. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mmoja wa wanaharakati wa Shirika la  Pax Christi ambayo inajishughulisha na harakati za amani nchini Ujerumani amesema kuwa, stratijia ya nyuklia ya Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) barani Ulaya, iliyojengeka juu ya msingi wa kulimbikiza silaha za nyuklia na mifumo ya kukabiliana na mashambulizi ya nyuklia, iko kinyume na mikataba ya kupiga marufuku silaha hizo hatari.

Maandamano hayo

Katika maandamano hayo taasisi ya amani ya kitiba ya IPPNW pamoja na kampeni ya dunia kwa ajili ya kuangamiza silaha za nyuklia zimetaka kufanyika kongamano la kimataifa kwa lengo la kuondolewa silaha za nyuklia za Marekani barani Ulaya. Uwepo wa silaha za Marekani katika ardhi ya Ujerumani umekuwa ukikabiliwa na malalamiko ya kila mara ya wananchi na kadhalika ukosoaji mkali wa wanasiasa wa nchi hiyo.