Amnesty yaikemea Marekani kwa kujiondoa katika Baraza la Haki za Binadamu
https://parstoday.ir/sw/news/world-i46114-amnesty_yaikemea_marekani_kwa_kujiondoa_katika_baraza_la_haki_za_binadamu
Katibu Mkuu wa shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International amekemea vikali hatua ya Marekani ya kujiondoa katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na kusema kuwa: Kwa mara nyingine tena Rais wa Marekani ameonesha jinsi asivyojali haki za bindamu na uhuru wa kimsingi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 20, 2018 22:40 UTC
  • Amnesty yaikemea Marekani kwa kujiondoa katika Baraza la Haki za Binadamu

Katibu Mkuu wa shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International amekemea vikali hatua ya Marekani ya kujiondoa katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na kusema kuwa: Kwa mara nyingine tena Rais wa Marekani ameonesha jinsi asivyojali haki za bindamu na uhuru wa kimsingi.

Salil Shetty amesema kuwa, japokuwa Baraza la Haki za Binadamu si kamili na utendaji wa wanachama wake umekuwa ukikosolewa lakini bado ni marejeo muhimu ya kutekeleza uadilifu.

Katibu Mkuu wa Amnesty International ameongeza kuwa: "Uamuzi wa Marekani wa kujiondoa katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa utaifanya nchi hiyo ilaumiwe na kuhukumiwa katika historia ya mwanadamu na kwa hatua hiyo, Marekani imeamua kwa makusudi kukanyaga haki za binadamu popote pale duniani.

Donald Trump

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo na balozi wa nchi hiyo katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley Jumanne iliyopita walitangaza uamuzi wa serikali ya Washington wa kujiondoa katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa. Hatua hiyo imechukuliwa na Marekani kwa shabaha ya kuulinda na kuutetea utawala haramu wa Israel unaolaumiwa kwa mara kwa mara kwa kuua na kukanyaga haki za raia wa Palestina.