Russia: Uchokozi wa Israel wa kutuulia watu wetu Syria lazima utajibiwa
https://parstoday.ir/sw/news/world-i48253-russia_uchokozi_wa_israel_wa_kutuulia_watu_wetu_syria_lazima_utajibiwa
Mbali na Rais Vladimir Putin na viongozi wengine mbalimbali wa kiserikali wa Russia kusisitizia wajibu wa kujibiwa mauaji yaliyofanywa na Israel dhidi ya wanajeshi wa nchi hiyo huko Syria, mkuu wa akademia ya masuala ya jeopolitiki ya Russia naye ametilia mkazo msimamo huo.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Sep 19, 2018 23:16 UTC
  • Russia: Uchokozi wa Israel wa kutuulia watu wetu Syria lazima utajibiwa

Mbali na Rais Vladimir Putin na viongozi wengine mbalimbali wa kiserikali wa Russia kusisitizia wajibu wa kujibiwa mauaji yaliyofanywa na Israel dhidi ya wanajeshi wa nchi hiyo huko Syria, mkuu wa akademia ya masuala ya jeopolitiki ya Russia naye ametilia mkazo msimamo huo.

Shirika la habari la Fars limemnukuu Leonid Ivachov, mkuu wa akademia ya masuala ya jeopolitiki ya Russia akisisitizia suala hilo na kusema, tab'an Russia haitofanya shambulizi la moja kwa moja dhidi ya viwanja vya ndege vya Israel, lakini inabidi jeshi la Syria liongezewe nguvu za kudhamini usalama wa anga yake na kutoruhusu ndege yoyote kuingia katika  anga yake bila ya ruhusa ya Damascus, vingonevyo itadondoshwa.

Viongozi wa Russia wamekasirishwa mno na kitendo cha utawala wa Kizayuni wa Israel cha kutuma ndege zake katika mkoa wa Ladhiqiyah (Latakia) nchini Syria na kupelekea kuangushwa ndege moja ya kijeshi ya Russia iliyokuwa na watu 15.

Ndege ya Russia aina ya Ilyushin 20

 

Kwa upande wake, Serguei Choigou, waziri wa ulinzi wa Russia amejibu uchokozi huo wa Israel kwa kutoa tamko rasmi na kusema kuwa, lawama za kuangushwa ndege ya Russia aina ya Ilyushin 20 huko Syria na kuuliwa watu waliokuwemo zinabebwa kikamilifu na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Waziri huyo wa ulinzi wa Russia alionesha ramani ya safari za ndege hizo na kusema kuwa, ndege za Israel ziliifanya ndege hiyo ya Russia kuwa ngao yake.

Kwa upande wake, mkuu wa akademia ya masuala ya jeopolitiki ya Russia vile vile amependekeza kuchukuliwa hatua nyingine mbalimbali dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel ikiwa ni pamoja na kuwapiga marufuku Wazayuni kutembelea Russia.