Washington Post: Marekani inaogopa nguvu za kijeshi za Iran
https://parstoday.ir/sw/news/world-i49275-washington_post_marekani_inaogopa_nguvu_za_kijeshi_za_iran
Gazeti la Washington Post limeashiria jinsi Marekani ilivyorudi nyuma kutoka eneo la Ghuba ya Uajemi katika miezi kadhaa iliyopita na kuripoti kuwa viongozi wa nchi hiyo wana wasiwasi kutokana na uwezo wa kijeshi wa Iran unaozidi kuongezeka.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 04, 2018 12:18 UTC
  • Washington Post: Marekani inaogopa nguvu za kijeshi za Iran

Gazeti la Washington Post limeashiria jinsi Marekani ilivyorudi nyuma kutoka eneo la Ghuba ya Uajemi katika miezi kadhaa iliyopita na kuripoti kuwa viongozi wa nchi hiyo wana wasiwasi kutokana na uwezo wa kijeshi wa Iran unaozidi kuongezeka.

Kwa mujibu wa Washington Post, wasiwasi wa viongozi wa Marekani umezidi kuongezeka kutokana na uamuzi wa wizara ya ulinzi ya nchi hiyo Pentagon wa kuzielekeza nje ya eneo la Ghuba ya Uajemi meli, ndege za kivita na mifumo ya ulinzi wa makombora, sambamba na kukaribia muda wa kuanza kuwekwa tena vikwazo dhidi ya Iran katika sekta ya nishati.

Washington Post limebainisha kuwa, kutokana na kubadilika vipaumbele vya usalama wa taifa vya Marekani katika serikali ya Trump, na kushughulishwa zaidi fikra za Ikulu ya White House na mashindano ya kijeshi kati ya nchi hiyo na China na Russia, harakati za Marekani katika Mashariki ya Kati zimepungua.

Kabla ya hapo, gazeti la Wall Street Journal liliwahi kuandika ripoti inayofanana na ile ya Washington Post kwa kueleza kwamba, licha ya kauli za uropokaji zilizotolewa mara kadhaa na viongozi wa Washington, vikosi vya jeshi la Marekani vimekuwa vikirudi nyuma kutoka eneo la Mashariki ya Kati.

Wanajeshi wa Marekani walipokamatwa na kupigishwa magoti na vikosi vya ulinzi vya Iran baada ya kuvuka mpaka wa majini wa Jamhuri ya Kiislamu

Kwa mujibu wa gazeti hilo, tangu mwezi Machi mwaka huu wa 2018, wakati manowari ya Theodore Roosevelt ilipoondoka eneo hili na kuelekea Bahari ya Pasifiki, hakuna manowari nyingine zozote za ushambuliaji za Marekani zilizoshuhudiwa katika Ghuba ya Uajemi.

Gazeti hilo limebainisha kuwa, katika kipindi cha miongo miwili iliyopita, hiki ni kipindi kirefu zaidi cha kutokuwepo manowari yoyote ya Marekani ya kubebea ndege katika maji ya Ghuba ya Uajemi. 

Kuwepo wanajeshi wa Marekani katika Ghuba ya Uajemi kunakofanyika kwa lengo la kuingilia masuala ya eneo hili kumekuwa kukikosolewa sana kila mara.../