John Bolton akiri kwamba Marekani haina uwezo wa kuishambulia kijeshi Iran
John Bolton, Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani amekiri kwamba nchi hiyo haina uwezo wa kukabiliana kijeshi na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Kanali ya televisheni ya CNBC imemnukuu Bolton ambapo licha ya kuitishia Iran kwamba Marekani inaweza kuishambulia kwa haraka sambamba na kutuma manowari inayobeba ndege za kivita katika eneo, lakini amelegeza msimao kwa kusema: "Tunaionya Tehran, lakini hatutaki kupigana vita." Kabla ya hapo Mshauri huyo wa Usalama wa Taifa wa Marekani alitoa vitisho kwamba, Marekani itatuma katika eneo manowari ya kivita ya USS Abraham Lincoln yenye uwezo wa kubeba ndege za kivita.
Inafaa kuashiria kuwa, siasa na hatua za kupenda kujitanua na vitisho za Marekani, zimekuwa zikikabiliwa na radiamali hasi ya serikali mbalimbali zikiwemo za Ulaya. Hii ni katika hali ambayo viongozi wa serikali ya Trump bado wanaendelea kutoa matamshi ya vitisho dhidi ya Iran. Mkabala wake Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, imekuwa ikisisitiza kwamba hatua za kupenda makubwa za Washington, zitapata jibu kali kutoka kwa nchi hii.