Ilhan Omar asisitiza kurejea White House katika makubaliano ya JCPOA
Mbunge Muislamu katika baraza la wawakilishi la Marekani amesema kuwa Washington inapasa kurudi kwenye meza ya mazungumzo na katika makubaliano ya nyuklia na Iran.
Ilhan Omar ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter kuwa Washington inapasa kurudi kwenye meza ya mazungumzo na katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA. Mbunge huyo katika baraza la wawakilishi la Marekani ameeleza kuwa Rais Donald Trump wa nchi hiyo hakupasa kujito katika makubaliano hayo ya nyuklia na Iran. Kuanzia Mei nane mwaka huu baada ya Marekani kujitoa katika makubaliano hayo ya nyuklia na kuanza kutekeleza vikwazo vyake vya upande vyake vya upande mmoja dhidi ya Tehran; Iran nayo imechukua hatua za kusimamisha baadhi ya hatua zake kuhusu makubaliano hayo ya nyuklia na kutoa muhula wa siku 60 kwa nchi zilizosalia kwenye makubaliano hayo ya nyuklia kutekeleza ahadi zao khususan katika sekta za kibenki na mafuta.
Behruz Kamalvandi Msemaji wa Taasisi ya Nishati ya Nyuklia ya Iran pia alisema jana katika kikao na waandishi wa habari kilichofanyika katika ofisi ya maji mazito ya Arak kuwa katika siku kumi zijazo itaongeza mara nne urutubishaji wa urani na hivyo kupindukia kiwango kilichoainishwa cha kilo 300.