Mfumo maalumu wa kifedha wa INSTEX waanza kufanya kazi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i54432-mfumo_maalumu_wa_kifedha_wa_instex_waanza_kufanya_kazi
Helga Schmid, Msaidizi wa Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, amesema kuwa mfumo maalumu wa mabadilishano ya fedha kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Umoja wa Ulaya, tayari umeanza kufanya kazi na hatua ya kwanza ya mabadilishano hayo inaendelea kufanya kazi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 28, 2019 23:50 UTC
  • Mfumo maalumu wa kifedha wa INSTEX waanza kufanya kazi

Helga Schmid, Msaidizi wa Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, amesema kuwa mfumo maalumu wa mabadilishano ya fedha kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Umoja wa Ulaya, tayari umeanza kufanya kazi na hatua ya kwanza ya mabadilishano hayo inaendelea kufanya kazi.

Helga Schmid ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba, kikao cha jana cha kamisheni ya pamoja kilifikia masuala jumla, na kwamba kilikuwa na matokeo chanya. Ameongeza kuwa hadi sasa mfumo wa kifedha wa INSTEX unafanya kazi na kwamba hatua ya kwanza ya mabadilishano inaendelea kutekelezwa. Aidha amesema kuwa wanachama wengi wa nchi za Ulaya watajiunga na mfumo huo. Aidha Msaidizi huyo wa Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, Bi Federica Mogherini ameutaja utekelezwaji athirifu na kamilifu wa mapatano ya nyuklia ya JCPOA na pande zote husika kuwa ni maudhui muhimu na kuongeza kuwa mafanikio pia yamefikiwa kuhusiana na miradi ya amani ya nyuklia ya Arak na Fordo.

Helga Schmid, Msaidizi wa Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya.

Kikao cha 12 cha kamisheni ya pamoja ya mapatano ya nyuklia ya JCPOA kilifanyika Ijumaa ya jana mjini Vienna Austria ikiwa zimesalia siku chache kabla ya kumalizika muhula wa siku 60 uliotolewa na Iran kwa ajili ya pande nyingine za mapatano hayo kutekeleza majukumu yao. Kikao hicho kilichodumu kwa muda wa zaidi ya saa tatu kwa kuwakutanisha pamoja manaibu waziri na wakuu wa kisiasa wa Iran na kundi la 4+1, kilihudhuriwa pia na Sayyid Abbas Araqchi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa pamoja na Helga Schmid, Msaidizi wa Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya. Hayo yanajiri katika hali ambayo nchi saba za Ulaya zikiwemo Austria, Sweden, Finland, Ubelgiji, Uholanzi, Slovania, Uhispania, zimetoa taarifa ya pamoja zikitaka kutekelezwa mfumo huo wa kifedha wa INSTEX kwa ajili ya kuikinaisha Iran iendelee kubakia katika mapatano ya JCPOA.