Donald Trump akaribishwa kwa maandamano ya maelfu ya watu nchini India
https://parstoday.ir/sw/news/world-i59356-donald_trump_akaribishwa_kwa_maandamano_ya_maelfu_ya_watu_nchini_india
Rais Donald Trump wa Marekani amekaribishwa nchini India kwa maandamano ya maelfu ya watu wanaopiga nara dhidi ya kiongozi huyo na siasa zake za kibaguzi na kijuba.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 24, 2020 04:47 UTC
  • Donald Trump akaribishwa kwa maandamano ya maelfu ya watu nchini India

Rais Donald Trump wa Marekani amekaribishwa nchini India kwa maandamano ya maelfu ya watu wanaopiga nara dhidi ya kiongozi huyo na siasa zake za kibaguzi na kijuba.

Vyombo vya habari vinasena kuwa, sambamba na kuwasili rais huyo wa Marekani nchini India, maelfu ya wananchi wamefanya maandamano wakieleza chuki na hasira zao dhidi ya kiongozi huyo ambaye wanasema ni mbaguzi.

Televisheni ya NDTV ya India imeripoti kuwa, Rais Donald Trump leo Jumatatu amewali katika mji wa Ahmedabad ambao ndio mkubwa zaidi wa jimbo la Gujarat huko magharibi mwa India na anatazamiwa kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa ndhi hiyo, Narendra Modi.

Safari ya sasa ya Trump nchini India inafuatia ile iliyofanywa na Modi mjini Washington mwezi Septemba mwaka jana. 

Safari hiyo ya Trump inafanyika huku New Delhi ikijitayarisha kununua zana za kijeshi zenye thamani ya dola bilioni 2.6 zikiwemo helikopta za kisasa kutoka kampuni ya Kimarekani ya Lockheed Martin.