Aliyehudhuria hotuba ya Trump aambukizwa Corona
https://parstoday.ir/sw/news/world-i59618-aliyehudhuria_hotuba_ya_trump_aambukizwa_corona
Matokeo ya vipimo vya virusi vya Corona alivyofanyiwa mmoja watu waliohudhuria kikao cha 'Umoja wa Wahafidhina wa Marekani' ambacho Trump na makamu wake walihutubia, yameonyesha kuwa mtu huyo ameathirika na virusi vya Corona.
(last modified 2026-02-05T09:20:29+00:00 )
Mar 08, 2020 08:38 UTC
  • Aliyehudhuria hotuba ya Trump aambukizwa Corona

Matokeo ya vipimo vya virusi vya Corona alivyofanyiwa mmoja watu waliohudhuria kikao cha 'Umoja wa Wahafidhina wa Marekani' ambacho Trump na makamu wake walihutubia, yameonyesha kuwa mtu huyo ameathirika na virusi vya Corona.

Baada ya vyombo vya habari kuripoti habari ya kuambukizwa watu wawili waliokuwepo kwenye kikao cha hivi karibuni cha lobi ya Wazayuni AIPAC mjini Washington, mshiriki mwingine wa kikao cha wiki ya kabla yake cha 'Umoja wa Wahafidhina wa Marekani' na kilichohutubiwa na Rais Donald Trump na makamu wake Mike Pence, amethibitika kuwa na maambukizi ya maradhi hayo. Ripoti hiyo imetolewa wakati ambao Trump amedai kuwa serikali yake imefanikiwa kufuatilia na kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona.

Virusi hatari vya Corona

Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) pia licha ya kuwa na mamia ya malaki ya askari katika maeneo tofauti ya dunia, hatimaye baada ya kupita miezi mitatu tangu kulipoibuka virusi vya Corona, imekiri kuwepo kesi ya kwanza ya waathiriwa wa ugonjwa huo kati ya askari wake ndani ya jimbo la Virginia. Andrew Cuomo, gavana wa jimbo la New York pia ameripoti kuwepo ongezeko jipya la waathirika wa virusi vya Corona kufikia watu 76 huku akiwaonya wale wanaouza kwa bei kubwa bidhaa za dharura za afya kutofanya hivyo. Kwa mujibu wa gavana huyo, huenda wahusika wakanyang'anywa vibali vyao vya biashara. Hadi sasa viongozi wa Marekani wametangaza vifo 19 kutokana na virusi vya Corona na karibu watu 500 tayari wameambukiwa maradhi hayo nchini humo.