Kim Jong-un, Kiongozi wa Korea Kaskazini aonekana hadharani
(last modified Sat, 02 May 2020 11:12:51 GMT )
May 02, 2020 11:12 UTC
  • Kim Jong-un, Kiongozi wa Korea Kaskazini aonekana hadharani

Shirika la Serikali ya Korea Kaskazini limeripoti habari ya kuonekana hadharani kiongozi wa nchi hiyo.

Shirika la Habari la KCNA limeripoti kwamba Kim Jong-un ameonekana wakati aliposhiriki katika sherehe ya ukamilishaji wa moja ya viwanda vya kuzalisha mbolea katika eneo la Pyongyang, mji mkuu wa nchi hiyo. Aidha Shirika la Habari la Reuters limetangaza kwamba, hii ni mara ya kwanza kwa kiongozi huyo wa Korea Kaskazini kufanya shughuli za wazi tangu tarehe 11 Aprili. Aidha shirika hilo limedai kwamba haliwezi kuthibitisha moja kwa moja habari hiyo.

Kim Jong-un akishiriki sherehe ya kukamilika kwa ujenzi wa moja ya viwanda

Katika wimbi la tetesi zinazohusiana na hali mbaya ya kiafya ya Kim Jong-un, gazeti la Rodong Sinmun linalochapishwa Korea Kaskazini Ijumaa liliandika kuwa, kiongozi wa nchi hiyo ametuma ujumbe kwa mnasaba wa Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) sambamba na kuwashukuru wafanyakazi wa nchi yake. Kutoonekana kiongozi huyo kijana katika macho ya watu kwa muda wa siku 20 kumepelekea kuibuka tetezi juu ya hali yake mbaya ya afya. Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 36 alionekana kwa mara ya mwisho tarehe 11 mwezi uliopita wakati aliposhiriki kikao na chama cha wafanyakazi na kutaka kuchukuliwa hatua kali za kukabiliana na virusi vya Corona.

Tags