Jul 29, 2020 02:29 UTC
  • Kushadidi malumbano ya kisiasa ya Umoja wa Ulaya na Uturuki

Kufuatia kushadidi taharuki baina ya Uturuki na Jordan, Kansela Angela Merkel wa Ujerumani, ambaye nchi yake inashikilia uwenyekiti wa kimzunguko wa Umoja wa Ulaya, amefanya mazungumzo na Rais Reccep Tayyib Erdogan wa Uturuki na kumtahadharisha kuwa, matatizo aliyonyao na Ugiriki hayataishia tu katika nchi hiyo bali atakumbana na matatizo na bara zima la Ulaya.

Uturuki na Ugiriki zina mzozo wa muda mrefu wa mpakani. Nchi hizo mbili ambayo ni wanachama wa muungano wa kijeshi wa NATO hata zimekaribia kuingia vitani mara kadhaa. Ugiriki ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya na Uturuki nayo pia inataka kujiunga na umoja huo. Ni kwa sababu hizo ndio nchi hizo hadi sasa zimechukua hatua za kujizuia kuzidisha uhasama na zinatumia njia laini kushinikizana.

Maudhui ya hivi karibuni ya mzozo baina ya nchi hizo ni hatua ya Uturuki ya kuanza mkakati wa kutafuta mafuta na gesi katika Bahari ya Mediterenia. Meli za utafiti za Uturuki wiki iliyopita zilianza shughuli katika Bahari ya Mediterenia. Ugiriki imepinga vikali hatua hiyo na imeweka jeshi lake katika hali ya tahadhari.

Huko nyuma pia Cyprus ambayo pia ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya ilikosolewa vikali na Uturuki baada ya kuanza uchumbaji gesi asilia mashariki mwa Bahari ya Mediterenia. Uturuki ni nchi pekee ambayo iliunga mkono kitendo cha kugawanyika Cyprus ambapo inaitambua ramsi Jamhuri ya Cyprus Kaskazini. Hitilafu za hivi karibuni baina ya Uturuki na Ugiriki ni sehemu ndogo tu ya hitilafu kubwa baina ya nchi hizo mbili na chimbuko lake ni kugawanyika Cyprus.

Radiamali ya Kansela Angela Merkel kuhusu hitilafu baina ya Uturuki na Ugiriki ni ishara ya kiwango cha hitilafu baina ya Umoja wa Ulaya na Uturuki.

Umoja wa Ulaya, hasa nchi kubwa na zenye ushawishi katika umoja huo kama vile Ujerumani, Ufaransa, Italia na Uhispani zimekuwa zikijaribu kutoingilia hitilafu baina ya Ugiriki na Uturuki na zimekuwa zikitoa wito kwa nchi hizo mbili kutulia na kufanya mazungumzo na hata zimejaribu kuzipatanisha. 

Baada ya Umoja wa Ulaya kusimamisha kwa muda mazungumzo ya Uturuki kujiunga na umoja huo kwa visingizio mbali mbali, Rais Erdogan amechukua misimamo huru ambayo haijaufurahisha Umoja wa Ulaya.

Katika kadhia ya Syria, Uturuki imejiondoa katika mrengo wa Marekani, Umoja wa Ulaya na uungaji mkono ISIS na sasa imejiunga na Iran, Russia pamoja na mhimili wa muqawama jambo ambalo limeibua changamoto kubwa katika uhusiano wa Uturuki na Umoja wa Ulaya.

Aidha Uturuki imeushinikiza Umoja wa Ulaya kwa kufungua mipaka yake na kuwaruhusu wakimbizi kumiminika Ulaya mara kwa mara.

Mirqasim Muumini, mtaalamu wa masuala ya Uturuki katika kubainisha upana wa mgogoro wa Uturuki na Ugiriki anasema hivi kuhusu iwapo mgogoro huo utaathiri muundo wa muungano wa kijeshi wa NATO: 'Iwapo nchi za Ulaya zitaamua kuunga mkono Ugiriki , basi zitafanya hivyo wazi wazi. Katika upande wa pili, iwapo Uturuki itajihisi imedhoofika, basi kwa mara nyingine itatitisha nchi za Ulaya kuwa itafungua mipaka yake ili wakimbizi wamiminiike Ulaya.

Nukta ya hivi karibuni ya hitilafu bauna ya Uturuki na Umoja wa Ulaya ni kuhusu Libya. Wakati ambao Umoja wa Ulaya unakosoa vikali hatua ya Uturuki  kuingilia kijeshi Libya, wakuu wa Uturuki wanakiuka wazi wazi vikwazo vya silaha dhidi ya Libya.

Ufaransa, Ujerumani na Italia zinasisitiza kuwa, kuendelea uingiliaji wa kijeshi wa Uturuki nchini Libya  kutapelekea Ankara iwekewe vikwazo na Umoja wa Ulaya. Hadi sasa Umoja wa Ulaya umejaribu kutumia njia na fursa zote kuishinikiza Uturuki ibadilishe sera zake kuhusu Libya na Afrika Kaskazini kwa ujumla. Ni kwa msingi huo ndio kinyume na ilivyo kuwa huko nyuma, ambapo Merkel alitumia lugha laini katika mgogoro wa Uturuki na Ugiriki, mara hii amekuwa mkali na amemuonya wazi wazi Erdogan kuhusu hatua zake za kuanzisha mkakati wa kuchimba mafuta na gesi  katika Bahari ya Mediterenia.

 

Tags