Hitilafu zaongezeka kuhusu kura za uchaguzi wa Rais nchini Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i64437-hitilafu_zaongezeka_kuhusu_kura_za_uchaguzi_wa_rais_nchini_marekani
Spika wa bunge la wawakilishi la Marekani amewaandikia barua wabunge wa chama cha Democratic akisistiza kuwa mgombea wa kiti cha urais wa chama hicho ana kura za kutosha za baraza maalumu la wajumbe wanaomchagua rais ( Electoral College) za kumfanya aibuke na ushindi na kuingia White House.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 05, 2020 04:28 UTC
  • Hitilafu zaongezeka kuhusu kura za uchaguzi wa Rais nchini Marekani

Spika wa bunge la wawakilishi la Marekani amewaandikia barua wabunge wa chama cha Democratic akisistiza kuwa mgombea wa kiti cha urais wa chama hicho ana kura za kutosha za baraza maalumu la wajumbe wanaomchagua rais ( Electoral College) za kumfanya aibuke na ushindi na kuingia White House.

Katika barua yake hiyo Bi Nancy Pelosi amesisitiza kuwa wananchi wa Marekani wamebainisha wazi takwa lao kupitia masanduku ya kura kwa kuwachagua Joe Biden na Kamalla Haris kuingia White House. Biden pia jana alasiri kwa wakati wa Marekani alitoa hotuba iliyoashiria ushindi wake kwa kusema: Nitakuwa rais wa nchi nzima; na nitawatumikia wananchi wote wa Marekani; iwe wale walionipigia kura au hata wale ambao hawakunipa kura. 

Nancy Pelosi, Spika wa bunge la Wawakilishi wa Marekani 

Wakati huo huo Rais Donald Trump ameandika katika ukurasa wake wa twitter kwamba: Wademocrat wanasaka kura za Biden katika majimbo ya Pennsylvania, Wisconsin na Michigan, 

Gazeti la Wall Street Journal limeandika kuwa pamoja na kuwa matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa rais Marekani bado hayajajulikana hadi sasa lakini timu ya Biden inajipanga kwa ajili ya kuchukua madaraka kutoka kwa Trump. Mahakama katika jimbo la Pennsylvania pia imepinga mashtaka yaliyowalishwa na timu ya kampeni ya Trump kuhusu namna uchaguzi  na zoezi la kuhesbu kura lilivyoendeshwa. 

Mratibu Maalumu wa Usimamizi wa Taasisi ya Usalama na Ushirikiano ya Ulaya pia amesema kuwa: Madai yasiyo na msing kuhusu mapungufu ya kimfumo khususan yaliyotolewa na Rais Donald Trump yanapunguza imani ya wananchi kwa taasisi za kidemokrasia. 

Maafisa husika katika jimbo hilo wamesisitiza pia kuwa hadi kura ya mwisho itahesabiwa licha ya matakwa ya Trump. Kulingana na kura zilizohesabiwa hadi sasa katika uchaguzi wa rais wa Marekani, Joe Biden mgombea wa kiti cha urais wa chama cha Democratic anaongoza kwa kuwa na kura 264 za Electoral College na Trump akiwa na kura 214. 

Donald Trump na Joe Biden 

Muda wa upigaji kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu nchini Marekani katika majimbo yote ya nchi hiyo ulimalizika jana usiku; na maafisa wa uchaguzi bado wanaendelea na zoezi la kuhesabu kura.