Sana'a: Marekani ni kinara wa ugaidi wa kimataifa
https://parstoday.ir/sw/news/world-i65730-sana'a_marekani_ni_kinara_wa_ugaidi_wa_kimataifa
Msemaji wa Serikali ya Wokovu wa Kitaifa ya Yemen amesema kuwa Marekani imetumia njia zote kwa ajili ya kuliangamiza taifa la Yemen na nchi hiyo ndio kinara wa ugaidi duniani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 12, 2021 09:43 UTC
  • Sana'a: Marekani ni kinara wa ugaidi wa kimataifa

Msemaji wa Serikali ya Wokovu wa Kitaifa ya Yemen amesema kuwa Marekani imetumia njia zote kwa ajili ya kuliangamiza taifa la Yemen na nchi hiyo ndio kinara wa ugaidi duniani.

Akijibu uamuzi wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani wa kuitaja harakati ya Ansarullah ya Yemen kuwa ni kundi la kigaidi, Zaifullah al Shami amesema kuwa: Marekani imefanya hivyo kutokana na hitilafu za ndani zinazoendelea kuisumbua nchi hiyo katika kipindi hiki cha kumalizika kipindi cha urais wa Donald Trump ambaye anafanya kila linalowezekana ili kuwapunguzia mashinikizo waitifaki wake yaani Saudi Arabia na Imarati.  

Al Shami amesema kitendo cha Marekani cha kuitaja harakati ya Ansarullah kuwa ni kundi la kigaidi kumeweka wazi kilele cha jinai zilizotekelezwa na nchi hiyo dhidi ya watu wa Yemen na kuongeza kuwa, kitendo hicho cha Marekani si tu hakiathiri mwelekeo wa kijeshi au kijamii wa vikosi vya Yemen bali kinazidisha nguvu na azma ya vikosi hivyo. 

Wanamuqawama wa Ansarullah ya Yemen 

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani, Mike Pompeo jana Jumatatu alitangaza kuwa, wizara hiyo imeifahamisha Kkngresi kuhusu umauzi wake wa kuiorodhesha harakati ya Ansarullah ya Yemen katika faharasa yake ya taasisi ya kigaidi duniani.