Utumiaji mabavu na mauaji vyaongezeka Canada
Licha ya serikali ya Canada kufanya jitihada za kupunguza machafuko na utumiaji mabavu nchini, nchi hiyo katika miezi ya karibuni imekumbwa na jinai na vitendo vingi vinavyohusiana na utumiaji wa silaha baridi na moto.
Katika jinai ya hivi karibuni, polisi ya Canada Jumapili iliyopita iliripoti kujiri mashambulizi ya utumiaji visu ambapo wahanga walipatikana katika eneo lenye wakazi asilia la James Smith Cree Nation na huko Weldon. Watu wasiopungua 10 waliuawa na wengine 15 kujeruhiwa katika tukio hilo lililowashtua wananchi wa Canada.
Justin Trudeau Waziri Mkuu wa Canada ameyataja mashambulizi hayo huko Saskatchewan kuwa ya kutisha na kuhuzunisha.
Mashambulizi hayo ya visu yaliyojiri Jumapili iliyopita katika jimbo la Saskatchewan ambapo si muda mrefu tangu kuchapishwa ripoti kuhusu uwepo wa mtu aliyejizatiti kwa silaha ya otomatiki karibu na shule katika mji wa Toronto nchini humo yamepelekea kufungwa shule nne na kuimarishwa ulinzi katika mji huo.
Wahusika wa mashambulizi hayo ya visu wametajwa kwa majina ya Damien and Myles Sanderson ndugu wawili walio na umri wa miaka 30 na 31.