Mar 25, 2023 02:20 UTC
  • Aliachwa akihangaika na kifo peke yake; Hasira zatanda Ufaransa baada ya kifo cha mwanafunzi mwenye asili ya Kiarabu

Mitandao ya kijamii nchini Ufaransa imeshuhudia wimbi kubwa la hasira na ghadhabu baada ya kifo cha mwanafunzi mwenye asili ya Kiarabu ambaye alipatwa na mshtuko wa moyo, huku kukiwa na shutuma kwamba uongozi wa shule ulimwacha akikabilina na kifo peke yake bila ya kumpa huduma ya dharura.

Vyombo vya habari vya Ufaransa vimefichua kuwa, kisa hicho kilianza wakati wanafunzi wote wa "sayansi na mbinu za usimamizi" katika shule ya upili huko Lille (kaskazini mwa nchi) walipokuwa katika mtihani wa sheria ya mazingira, wakati Nazir (19) alipozirai na kuanguka chini.

Gazeti la The Voice of the North limemnukuu Vincent, mwanafunzi wa shule hiyo ya upili, akisema kwamba Nazir alipoteza fahamu mara moja, na wanafunzi wenzake walipokwenda kumsaidia, waliamriwa kumuacha na kurudi kwenye viti vyao.

Mwanafunzi mwingine wa shule hiyo ya sekondari amesema: "Nazir" aliachwa chini kwa muda, kabla ya rangi yake kubadilika, na baada ya hapo mshauri wa elimu aliitwa, ndipo timu za ulinzi wa raia zilipokuja na kumchukua kijana huyo hospitali, na kujaribu kumwokoa, lakini majaribio yote yalishindwa."

Mwanaharakati Siham Asbagh amehoji - kupitia akaunti yake ya Twitter - kwamba: "Je, watu wazima waliokuwapo hapo waliambiana nini kumwacha mtu anayepambana na kifona chini na kuwataka wanafunzi wenzake kuendelea na mitihani yao?"

Wanaharakati wa mtandao wa kijamii wa Twitter wameutuhumu uongozi wa shule hiyo kuwa umefanya ubaguzi kwa kumwacha mwanafunzi mwenye asili ya Kiarabu, "Nazir" katika hali hiyo hadi akafariki dunia.

Vitendo vya ubaguzi hususan dhidi ya Waislamu vimekuwa vikiripotiwa kwa wingi katika nchi za Ulaya hususan Ufaransa ambako idadi ya Waislamu ndiyo kubwa zaidi kati ya nchi zote za Ulaya. 

Tags