Jun 24, 2016 03:07 UTC
  • Takwimu kuhusu matukio ya ufyatuaji risasi nchini Marekani

Takwimu mpya zinaonyesha kujiri matukio 50 ya ufyatuaji risasi katika majimbo tofauti huko Marekani katika kipindi cha masaa 24 pekee.

Takwimu zilizotolewa jana (Alkhamisi) kuhusu matukio ya ufyatuaji risasi yaliyojiri nchini Marekani zinaonyesha kuwa watu 13 wameuawa na wengine 45 kujeruhiwa katika matukio 50 ya ufyatuaji risasii yaliyojiri katika muda saa 24 pekee katika majimbo mbalimbali ya Marekani.

Takwimu kuhusu matukio ya kutumia mabavu na utumiaji silaha huko Marekani pia zinaonyesha kuwa, watu watatu wameuliwa na mmoja kujeruhiwa katika tukio baya zaidi la ufyatuaji risasi lililotokea katika jimbo la Lease huko Washington katika muda huo.

Chanzo cha ufaytuaji risasi huo bado hakijafahamika na hadi tunaandaa habari hii, mshukiwa au washukiwa wa tukio bado walikuwa bado hawajatiwa mbaroni.

Aidha katika tukio jingine lililotokea huko Chicago, watu wanne wamejeruhiwa baada ya mtu mmoja aliyekuwa na silaha kuwafyatulia risasi. Mtu huyo aliyekuwa na silaha aliwauwa watu hao kwa kuwapiga risasi kutoka garini.

Kitengo cha takwimu za utumiaji silaha cha Marekani Jumatatu wiki hii kilitoa ripoti yake iliyoonyesha kuwa tangu kuanza mwaka huu wa 2016 hadi hivi sasa, kumejiri matukio 24,532 vya ufyatuaji risasi nchini humo; ambapo watu 6,303 wameuawa na wengine 12,952 kujeruhiwa.

Tags