-
Waislamu wa India wapinga kuondolewa kwenye orodha ya wapiga kura kwa kisingizio kwamba wamekufa
Jan 20, 2026 06:52Waislamu wa India wamefanya maandamano katika mji wa Ahmedabad, kupinga kuondolewa majina yao kwenye orodha ya wapiga kura kwa kisingizio kwamba wamefariki dunia, ingawa bado wako hai.
-
Viongozi mashuhuri wa kidini Marekani walaani sera ya kigeni ya serikali ya Trump
Jan 20, 2026 06:51Viongozi kadhaa wakuu wa Kanisa Katoliki nchini Marekani wametoa taarifa wakikosoa vikali sera ya mambo ya nje ya Washington na kusema kwamba nafasi yake ya kimaadili katika jukwaa la kimataifa inatiliwa shaka, kuhusiana na migogoro kama ya Ukraine, Venezuela na Greenland.
-
Michael McCaul: Uvamizi wa Marekani dhidi ya Greenland una maana ya vita na NATO/The Economist: Uchoyo wa Trump utaiangamiza NATO
Jan 20, 2026 02:03Mbunge mmoja wa Marekani ameutaja uvamizi wa nchi hiyo dhidi ya Greenland kuwa utakuwa "vita dhidi ya Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi, NATO."
-
Greenland na mantiki ya ubabe; ushuru, wenzo wa mashinikizo ya kisiasa ya Trump
Jan 18, 2026 23:26Rais Donald Trump wa Marekani ametangaza kuwa, kuanzia Februari Mosi, ataweka ushuru wa 10% kwa nchi zinazopinga kuunganishwa Greenland na Marekani na kwamba, kuanzia tarehe Mosi Juni ushuru huo utaongezwa na kufikia 25%.
-
Pentagon kutuma wanajeshi 1,500 kukabiliana na waandamanaji Minnesota
Jan 18, 2026 23:10Wizara ya Vita ya Marekani (Pentagon) imewaamuru wanajeshi wapatao 1,500 walio kazini wawe tayari kutumwa kwenda kukandamiza maandamano huko Minnesota.
-
Rais wa muda: Venezuela ina haki ya kujenga uhusiano na Iran
Jan 18, 2026 23:08Rais wa uongozi wa muda wa Venezuela, Delcy Rodriguez, amethibitisha tena kwamba Caracas ina haki ya kudumisha uhusiano wa kidiplomasia na China, Cuba, Iran na Russia na kupinga uingiliaji wa Marekani. Rais wa serekali muda ya Venezuela pia amekosoa hatua za kichokozi za Washington dhidi ya nchi hiyo.
-
Wakazi wa Greenland waandamana kupinga vitisho vya Trump
Jan 18, 2026 06:54Wakazi wa Greenland walifanya maandamano jana Jumamosi kupinga azma ya Rais wa Marekani Donald Trump ya kutaka kisiwa hicho cha Aktiki kikabidhiwe Washington, wakisisitiza kuwa wakazi wa eneo hilo wanapasa kuachwa waamue mustakabali wa kisiwa hicho.
-
Trump auza viti vya 'Bodi ya Amani' Gaza dola bilioni 1
Jan 18, 2026 06:54Rais wa Marekani, Donald Trump amezitaka nchi mbali mbali duniani zilipe angalau dola bilioni 1 ili kusalia katika "Bodi ya Amani" ya Gaza, baada ya kumalizika muhula ulioanishwa wa miaka mitatu.
-
Wananchi Pakistan, Iraq waandamana kuiunga mkono Iran, Kiongozi Muadhamu
Jan 18, 2026 03:34Wananchi katika nchi za Pakistani na Iraq wamefanya maandamano kuiunga mkono Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei mbele ya vitendo vya kigaidi vya hivi karibuni vilivyofadhiliwa na Marekani, Israel na madola mengine ya kibeberu.
-
NGOs za Uingereza zaitaka serikali kusitisha mauzo yote ya silaha kwa utawala wa Israel
Jan 17, 2026 23:07Muungano wa mashirika yasiyo ya kiserikali ya Uingereza (NGOs) umeitaka serikali ya nchi hiyo kusitisha uuzaji wa silaha kwa utawala wa Israel, na kuonya kuwa silaha zinazotengenezwa Uingereza ziko hatarini kutumika katika mauaji ya kimbari na kuzidi kumomonyoa sheria za kimataifa.