-
Vatican, Mexico nazo pia zaukataa uanachama katika 'Bodi ya Amani' ya Trump
Feb 18, 2026 07:00Vatican haitashiriki katika mpango wa Rais wa Marekani Donald Trump wa iitwayo "Bodi ya Amani". Hayo yameelezwa na afisa mkuu wa kidiplomasia wa Vatican Kardinali Pietro Parolin, huku akisisitiza kwamba juhudi za kushughulikia hali za mgogoro inapasa zisimamiwe na Umoja wa Mataifa.
-
Waziri Mkuu wa Slovakia: EU iko katika hali mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika historia yake
Feb 18, 2026 06:56Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico ameonya kwamba Umoja wa Ulaya (EU) sasa hivi unakabiliwa na hali mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika historia yake, huku matatizo ya kiuchumi yakizidishwa na kukosekana uongozi na maono ya muda mrefu huko Brussels.
-
Baadhi ya Waislamu waanza funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani
Feb 18, 2026 02:54Baadhi ya nchi za Waislamu na Kiarabu zimetangaza leo Jumatano kuwa siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
-
Kremlin: Jeshi la majini la Russia kuzima 'uharamia' wa Magharibi
Feb 18, 2026 02:54Afisa mwandamizi wa Ikulu ya Russia (Kremlin) ameonya kwamba, yumkini jeshi la wanamaji la nchi hiyo likatumwa kuzuia mataifa ya Magharibi kukamata meli za Urusi kama sehemu ya vikwazo dhidi ya usafirishaji wa mafuta ya Moscow.
-
Wataalamu wa UN waonya kuhusu hatari zinazowakabili waathirika wa "Mafaili ya Epstein"
Feb 17, 2026 23:35Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wamesema, wana wasiwasi mkubwa kuhusu madhara yanayoweza kuwapata waathirika waliotajwa katika nyaraka zinazojulikana kama "Mafaili ya Epstein" (Epstein Files), na kueleza kwamba mchakato wa utoaji wa taarifa hizo haukulinda ipasavyo faragha na usalama wao.
-
UN yatoa wito mpya wa kutokomeza ukoloni
Feb 17, 2026 07:09Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema ingawa zaidi ya mataifa 100 yamepata uhuru tangu mwaka 1945, mchakato wa kuondoa ukoloni bado haujakamilika. Ametoa kauli hiyo akifungua kikao cha mwaka 2026 cha Kamati Maalum ya Umoja wa Mataifa kuhusu Kutokomeza Ukoloni,
-
Kallas: Estonia inaipiku Marekani katika uhuru wa kujieleza
Feb 16, 2026 06:41Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, Kaja Kallas amepuuzilia mbali ukosoaji wa Washington kuhusu mbinyo wa kutoa maoni katika nchi wanachama wa umoja huo, akisisitiza kwamba nchi yake ya asili ya Estonia ina uhuru mkubwa zaidi wa kujieleza kuliko Marekani.
-
Je, China ina msimamo gani kuhusu hatua mpya za utawala wa Israel katika Ukingo wa Magharibi?
Feb 16, 2026 00:05China sambamba na kuashiria kuidhinishwa kanuni mpya na baraza la mawaziri la usalama la Israel ili kuimarisha udhibiti wa Ukingo wa Magharibi, imeonya kuhusu matokeo mabaya ya hatua hiyo.
-
Kutoka Kongamano la Usalama hadi "Sarakasi ya Munich"; Msimamo wa Iran Kuhusu Matukio ya Ulaya
Feb 15, 2026 04:48Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa: Ni jambo la kusikitisha kuona kwamba Kongamano la Usalama la Munich ambalo kwa kawaida huzingatiwa kuwa tukio muhimu na lenye hadhi kubwa, limegeuka kuwa "sarakasi ya Munich" kuhusu masuala ya Iran.
-
China: Tofauti kati ya Iran na Marekani zinapaswa kutatuliwa kupitia mazungumzo
Feb 14, 2026 23:19Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa China amesisitiza kuwa, tofauti kati ya Iran na Marekani zinapaswa kutatuliwa kupitia mazungumzo na upatanishi, na akaonya kwamba mvutano kati ya nchi hizo mbili unaweza kuathiri moja kwa moja amani na utulivu katika Asia Magharibi.