Sep 17, 2025 02:18 UTC
  • Jumatano, 17 Septemba 2025

Leo ni Jumatano tarehe 24 Mfunguo Sita Rabiul Awwal 1447 Hijria sawa na Septemba 17, 2025.

Siku kama ya leo miaka 77 iliyopita, aliaga dunia Emil Ludwig mwandika wasifu wa Kijerumani. Alizaliwa 1881 katika mji wa Breslau nchini Ujerumani ambao leo hii ni sehemu ya ardhi ya Poland. Alipata umashuhuri katika nusu ya pili ya karne ya 19 baada ya kuandika wasifu wa Otto Van Bismarck Kansela wa wakati huo wa Ujerumani, kiongozi wa zamani wa Russia Joseph Stalin, Beethoven na rais wa zamani wa Marekani Franklin Roosevelt. Wakati wa Vita vya Pili vya Dunia Ludwig alikuwa mwandishi wa habari aliyepata nafasi ya kufanya mahojiano na watawala waliokuwa na satua na ushawishi mkubwa katika kipindi hicho kama Franklin Delano Roosevelt, Winston Churchil na Joseph Stalin. 

Emil Ludwig

Tarehe 17 Septemba miaka 64 iliyopita aliuawa Waziri Mkuu wa zamaji wa Uturuki, Adnan Menderes. Alizaliwa mwaka 1899 na kupata elimu katika taaluma ya sheria. Alijiunga na harakati za kisiasa akiwa bado kijana na alishika hatamu za uongozi nchini Uturuki kama waziri mkuu mwaka 1950. Menderes ambaye alikuwa akifuata siasa za sera za kimarekani, alituma vikosi vya jeshi kushambulia Wakurdi wa nchi hiyo, suala ambalo liliwakasirisha sana wasomi na wanafikra wengi nchini Uturuki. Mwaka 1957 alichaguliwa tena kuwa Waziri Mkuu wa Uturuki na kukandamiza maandamano ya wanafunzi wa vyuo vikuu waliokuwa wakipinga utawala wake na kudai marekebisho ya kisiasa. Mwaka 1960 Adnan Menderes aliondolewa madarakani katika mapinduzi ya kijeshi na kufikishwa mahakamani ambapo alihukumiwa kifo kwa kupatikana na hatia ya kuua wanafunzi wa vyuo vikuu, kukiuka katiba ya nchi na kuwa na mahusiano haramu. Usiku wa kutekelezwa hukumu ya kifo, Menderes alifanya jaribio la kujiua lakini madaktari waliwahi kuokoa maisha yake. Hatimaye tarehe 17 Septemba, Adnan Menderes alinyongwa akiwa na umri wa miaka 62. 

Adnan Menderes  

Tarehe 26 Shahrivar miaka 45 iliyopita kwa mujibu wa kalenda ya Hijria Shamsia,  Saddam dikteta wa Iraq aliyeondolewa madarakani alibatilisha kwa upande mmoja makubaliano ya mipaka ya mwaka 1975 yaliyojulikana kwa jina la Mkataba wa Algeria kati yake na Iran. Siku hiyo, Saddam Hussein kiongozi wa zamani wa Iraq aliuchana mkataba huo wa Algeria mbele ya kamera za televisheni akiungwa mkono na madola ya kibeberu. Mkataba huo wa mwaka 1975 wa Algeria yalikuwa makubaliano ya mwisho kati ya nchi hizo mbili kwa ajili ya kutatua hitilafu za mipaka. Siku kadhaa baadaye, Saddam Hussein alianzisha uvamizi wa miaka minane dhidi ya ardhi ya Iran kwa uchochezi wa nchi za Magharibi. 

 

 Na Miaka 11 iliyopita tarehe 26 mwezi Shahrivar mwaka 1393 hijria shamsiya kwa mujibu wa kalenda ya Iran aliaga dunia Ahmad Bigdeli mwandishi mashuhuri wa riwaya wa zama hizi wa Iran. Alizaliwa tarehe 16 mwezi Farvardin mwaka 1324 hijria shamsiya sawa na mwaka 1945 miladia na alikuwa akiandika vitabu tangu miaka ya themanini miladia hadi alipoaga dunia. Riwaya yake ya "Kivuli Kidogo" ilimpatia Tuzo ya Kitabu cha Mwaka cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Marehemu Bigdeli alipata mafunzo katika Kitivo cha Sanaa ya Tamthilia. Baadhi ya riyawa za mwandishi mashuhuri Ahmad Bigdeli ni pamoja na hizi alizozipa majina ya "A Night Away from Home" cha mwaka 1995 na "I Am Destroyed" cha mwaka 2002. 

Ahmad Bigdeli