Dec 05, 2016 03:55 UTC
  • Jumatatu, Disemba 5, 2016

Leo ni Jumatatu tarehe 5 Mfunguo Sita Rabiul Awwal sawa na 5 Disemba 2016.

Siku kama ya leo miaka 3 iliyopita, alifariki dunia shujaa wa mapambano ya ukombozi na kupinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela akiwa na umri wa miaka 95. Mandela alizaliwa mwaka 1918 na alitumia zaidi ya nusu ya umri wake akipambana na utawala wa kibaguzi nchini kwake. Utawala wa wazungu wabaguzi ulimfunga jela kwa kipindi cha miaka 27 hadi mfumo wa ubaguzi wa rangi ulipofutwa mwaka 1990. Mwaka 1994 wananchi wa Afrika Kusini walimchagua Mandela kuwa Rais wa kwanza mzalendo wa nchi hiyo. Mwaka 1993 Mandela alitunukiwa tuzo ya amani ya Nobel. ***

Miaka 20 iliyopita katika siku kama ya leo, mtayarishaji filamu mashuhuri wa Iran, Ali Hatami aliaga dunia. Baada ya kuhitimu masomo katika Chuo cha Sanaa hapa nchini Hatami alijiunga na televisheni ya taifa na kujishughulisha na masuala ya filamu. Filamu zake nyingi ziliakisi mapenzi yake kwa utamaduni wa Iran. Miongoni mwa filamu hizo ni Sattarkhan, Sutedelan, Kamalul Mulk na Maadar.

Nelson Mandela

Katika siku kama ya leo miaka 146 iliyopita, aliaga dunia Alexander Dumas mwandishi mtajika wa Kifaransa. Mwandishi huyo ambaye ni mashuhuri pia kwa jina la Dumas Baba baada ya kumaliza masomo yake aliajiriwa katika ofisi moja ya kiwanda kama katibu kutokana na kuwa na hati nzuri.

Alexander Dumas

Siku kama ya leo miaka 142 iliyopita, Iran ilijiunga na Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu. Jitihada za awali za Iran kutaka kujiunga na shirika hilo zinarejea nyuma katika kipindi cha utawala wa Mfalme Nassereddin Shah Qajar. Katika kipindi cha utawala wake, Disemba 1874 Iran iliukubali mkataba uliopasishwa Geneva Uswisi, lakini licha ya kupita miaka kumi tangu isaini mkataba huo, utawala wake haukuchukua hatua yoyote ile ya kuasisi taasisi au jumuiya ambayo itatekeleza hati ya mkataba huo hapa Iran.

Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu

Tarehe 5 Disemba miaka 115 iliyopita alizaliwa Walt Disney shakhsiya mashuhuri wa sekta ya filamu za watoto. Disney alizaliwa katika mji wa Chicago huko Marekani. Walt Disney alihitimu masomo katika Chuo Kikuu cha Havard na kutunukiwa shahada ya udaktari katika sayansi ya uchoraji na uchongaji (Fine Art). Disney alitoa mchango mkubwa katika kuimarisha sanaa ya filamu za katuni. Mara kadhaa alitunukiwa tuzo za Oscar katika uwanja huo wa kutengeneza filamu za katuni. Miongoni wma kazi muhimu za Walt Disney ni Snow White, The Seven Dwarfs, Polar Bears.

Walt Disney

Miaka 36 iliyopita katika siku kama hii ya leo alikufa shahidi rubani Ahmad Keshvari. Brigedia Ahmad Keshvari aliingia katika Jeshi la Anga la Iran mwaka 1351 Hijria Shamsia na kuhitimu mafunzo ya kuendesha helikopta. Baada ya ushindi wa Mapindizi ya Kiislamu nchini mwaka 1979 alitoa mchango mkubwa katika kupambana na makundi yaliyokuwa dhidi ya mapinduzi katika maeneo ya magharibi mwa Iran na baadaye kidogo aliteuliwa kuwa kamanda wa jeshi la anga katika eneo la Ilam. Baada ya jeshi la Saddam Hussein kuvamia ardhi ya Iran, Brigedia Keshvari alikuwa mstari wa mbele kupambana na jeshi la adui na kulisababishia hasara kubwa ya nafsi na mali. Ahmad Keshvari aliuawa shahidi baada ya kukamilisha operesheni iliyokuwa na mafanikio akiwa njiani kurejea nchini.

Brigedia Ahmad Keshvari

 

Tags