Seli shina zatumika kutibu macho yaliyopoteza uwezo wa kuona
Hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni kujiunga nami katika makala nyingine yenye kuangazia maendeleo ya Iran katika sekta za sayansi, teknolojia na tiba nchini Iran na maeneo mengine duniani. Katika makala ya leo tutaangazia mafanikio ya wanasayansi Wairani katika kuunda lami isiyo na mada chafuzi kati ya mafanikio mengine. Karibuni kujiunga nami hadi mwisho.
Wanasayansi Wairani wamefanikiwa kuunda lami ambayo mada zake chafuzi zimeguezwa kuwa molekuli ambazo hazina madhara kwa mazingira. Mradi huu mpya wa teknolijia mpya ya kuzalisha lami ya barabara na lami ya kufunika paa za nyumba unajumuisha kubadilisha mada chafuzi za hydrocabron kuwa mada zisizo na madhara maji, carbon dioxide na oxigeni. Mafanikio haya yameweza kufikiwa na watafiti wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Azad mjini Ahvaz kusini mwa Iran. Mafanikio haya ni muhimu hasa kwa kuzingatia kuwa Iran ni kati ya nchi 4 zinazozalisha lami kwa wingi duniani na ya kwanza Mashariki ya Kati.
Daktari Ibrahim Panahpur, mtekelezaji wa mradi huo anafafanua zaidi kwa kusema: "Utafiti tuliofanya katika mradi huu umetegemea uchunguzi uliobaini kuwa wakati wa uchimbaji mafuta asilimia 75 ya gesi za hydrocaboni hupotea katika matope na pia katika mchanga ulio maeneo ya kuchimbwa mafuta, asilimia 90 ya mada chafuzi zilizogunduliwa husafishwa na kutoweka.."

Wataalamu wa masuala ya uchafuzi wa hewa wanasema mradi huu unaweza kutekeleza na iwapo utafanikiwa ilivyppangwa, bei ya mwisho ya kila mita mraba ya lami itauzwa karibu senti 50 dola. Mradi huu unatumia madini ambayo yanapatikana Iran. Teknolojia hii inaweza kutumia kutegeneza lami, isogamu au lami ya kufunika paa zisivuje maji n.k.
Katika mafanikio mengine, wanasayansi Wairani, mkuu wa kituo cha utafiti wa upasuaji wa mishipa katika Chuo Kikuu cha Tiba cha Mashhad kaskazini mashariki mwa Iran amesema wamegundua mbinu ya kutumia seli shina kutibu maumivu katika mishipa ya eneo la chini la miguu. Daktari Hassan Ravari anasema seli shina zinatumika kwa njia ya Angioplasty katika kutibu watu wenye matatizo ya mishipa katika eneo la chini ya miguu. Anasema majaribio ya matibabu hayo yamefanyiwa wagonjwa 20 na kwamba matokeo yatatangazwa hivi karibuni.

Daktari Ravari anasema mbinu hii ya tiba ni mpya kabisa na ndio inaanza kutumiwa duniani kwani inazuia kubanwa tena mishipa ya watu ambao wametibiwa kwa njia ya Angoplasty. Anaongeza kuwa seli shina ndizo zilizotumika kufanikisha mbinu hii mpya ya matibabu.
Katika habari nyingine, wanasayansi Wairani wamefanikiwa kuunda chombo au mashine ya kuzalisha oxygeni ndani ya nyumba. Mashine hii imetengenezwa kwa msaada ya Idara ya Sayansi na Teknolojia katika ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Mradi huu ni sehemu ya mradi mkubwa wa kitaifa wa teknolojia wenye lengo la kuzalisha hapa nchini mashine na bidhaa za kitiba zinazofanana na zile za mataifa ya kigeni yaliyoendelea kiviwanda. Kwa mujibu wa mradi huo maalumu, mashine kama hizo zinapaswa kuwa za kiwango cha juu na zizalishwe hapa nchini sambamba na kuwa na uwezo wa kushindana na mashine kama hizo za kigeni katika soko la kimataifa.
Mashine ya kuzalisha oxigeni iliyozalishwa na wataalamu wa Iran inaweza kushindana na mashine kama hizo ambazo zimekuwa zikiingizwa hapa nchini hutoka nchi za kigeni. Mashine hii ina umuhimu mkubwa katika kuwatibu watu wenye magonjwa mbali mbali ya kupumua na hivyo inapunguza gharama kutokana na kuzalishwa hapa nchini. Watu wenye matatizo ya kupumua kwa kawaida huhitajia oxigeni halisi muda wote na hulazimika kutumia chombo za kuzalisha oxigeni ili wabakie hai. Chombo hiki hasa nchini Iran hutumiwa na mavetarani wa vita vya miaka minane ambao waliathrika na mabomu ya kemikali za sumu yaliyorushw ana adui. Aidha mashine hii ya kuzalisha oxigeni pia hutumiwa sana na wenye matatizo ya mapafu, moyo, asma na wagonjwa wengine ambao kwa sababu moja au nyingine wanahitajia mashine ya oxigeni.

Kuundwa mashine hii nchini Irna kumefanyika baada ya uchunguzi wa kina wa kisayansi kuhusu mashine mshabaha za kigeni na baada ya hapo wanasayansi Wairani wakafanikiwa kuunda mashine hiyo kwa kutegemea teknolojia ya hapa nchini. Vipuri vya mashine hii pia vinazalishwa hapa nchini na tayari imeshafanyiwa majaribio katika maabara na hivi sasa kwa msaada wa Idara ya Sayansi na Teknolojia katika ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeanza kuzalishwa kwa wingi kiviwanda.
Hivi karibuni pia wanasayansi Wairani wamefanikiwa kuunda chombo cha kupima kiwango cha kasi, masafa na mpigo wa moyo wa wanariadha wakati wakiwa katika harakati. Vipimo vya chombo hiki ni vya uhakika na havina makosa na hivyo hutumiwa na makocha wa wanariadha na wanamichezo.
Chombo hiki kilichoundwa na wanasayansi Wairani mbali na kupima kasi, mpigo wa moyo na masafa ya mwanariadha pia kina uwezo wa kubaini iwapo hatua zinazopigwa na mawanriadhazina makosa au la. Halikadhalika chombo hiki kinaweza kupima kiwango cha kalori zilizochomwa wakati wa mazoezi.

Mohammad Heidari, msimamizi wa mradi huu anabainisha zaidi kwa kusema: "Hivi sasa kuna chombo kama hichi ambazo kimetengenezwa katika nchi za kigeni lakini kuna baadhi ya kazi ambazo hakiwezi kufanya wakati mwanariadha anapokitumia akiwa anakimbia au kufanya mazoezi. Na pia kwa chombo kilichopo cha kigeni kinategemea satalaiti ya GPS, katika maeneo ambayo satalaiti hiyo haina mawimbi, chombo hicho hakiwezi kufanya kazi." Anasema chombo kilichoundwa Iran kinaweza kufanya kazi hata sehemu ambazo hakuna GPS na hivyo kukifanya kiwe bora zaidi na fauka ya hayo kinauzwa kwa bei nafuu.
Na wanasayansi nchini Japan hivi karibuni wamefanikiwa kutumia seli shina kutibu macho ambayo yalikuwa yamefika kiwango cha kupoteza uwezo wa kuona pasina kuwepo matumaini ya kurejea katika hali ya kawaida. Awali utafiti huo ulifanywa katika panya ambao walikuwa wamepoteza uwezo wa kuona na kwa kutumia seli shina wakawaweza kupata uwezo wa kuona tena.

Kufuatia uchunguzi huo, mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu, kwa mara ya kwanza duniani mwanamue mmoja wa Japan mwenye umri wa miaka 60 alipokea retina ya jicho iliyokuzwa kwa kutumia seli shina za mtu mwingine na kuweza kutibiwa ugonjwa wa kupoteza uwezo wa kuona ujulikanao kama macular degeneration ambao huwaathiri zaidi wazee. Ugonjwa huo ukiendelea hupelekea muathirika hatimaye kupoteza uwezo wa kuona.
Daktari Masayo Takahashi kutoka Hospitali Kuu ya Mji wa Kobe City nchini Japan amesema oparesheni hiyo ilifanikiwa na sasa watasubiri muda wa mwaka moja kuona iwapo oparesheni hiyo imefanikiwa kikamilifu.
Ugonjwa huo wa macular degeneration unawaathiri watu milioni 170 duniani na hivyo mafanikio ya oparesheni hiyo ya Japan yatakuwa na matumaini kwa watu wengi kupata uwezo wao kuona tena.