May 25, 2017 04:26 UTC
  • Alkhamisi, 25 Mei, 2017

Leo ni Alkhamisi tarehe 28 Shaaban 1438 Hijria sawa na tarehe 25 Mei mwaka 2017 Miladia.

Katika siku kama ya leo miaka 54 iliyopita, hati ya Muungano wa Nchi Huru za Afrika OAU ilitiwa saini kwa kuhudhuriwa na nchi 30 za Kiafrika na kwa utaratibu huo kukawa kumeandaliwa uwanja wa kuasisiwa taasisi ya kuziunganisha pamoja nchi za Kiafrika.  Waasisi wa jumuiya hiyo walikuwa, Marais Jamal Abdul Nasser wa Misri, Kwame Nkrumah wa Ghana na Ahmed Sekou Toure wa Guinea. Jumuiya hiyo ilifanya jitihada za kuleta umoja baina ya nchi wanachama, kuzikomboa nchi zilizokuwa chini ya ukoloni na kutatua hitilafu pamoja na mifarakano baina ya nchi wanachahama. Mwaka 2000 viongozi wa OAU walikutana nchini Afrika Kusini na kubadilisha jina la taasisi hiyo muhimu barani Afrika na kuwa Umoja wa Afrika (AU). Hivi sasa umoja huo una wanachama 54 na makao yake makuu yapo mjini Addis Ababa Ethiopia. Siku hii ya tarehe 25 Mei inajulikana pia kwa jina la Siku ya Afrika. ****

Umoja wa Afrika

Katika siku kama ya leo miaka 657 iliyopita, kundi la mabaharia kutoka Ufaransa liliigundua Ghuba ya Guinea. Ghuba ya Guinea ipo magharibi mwa bara la Afrika katika bahari ya Atlantic. Takwimu za historia zinaonyesha kuwa, hakikupita kipindi kirefu tangu kugunduliwa ghuba hiyo, kabla ya Wafaransa hawajaanza upenyaji wao barani Afrika na taratibu wakaidhibiti ardhi iliyokuja kujulikana baadaye kwa jina la Guinea. Hatimaye mwaka 1958 Guinea ilijipatia uhuru baada harakati na mapambano ya wanaharakati na wapigania uhuru wa nchi hiyo  kuzaa matunda. ****

Ghuba ya Guinea

Miaka 125 iliyopita katika siku kama ya leo, alizaliwa Josip Broz Tito kiongozi wa zamani wa Yugoslavia. Tito alitiwa mbaroni mwaka 1915 wakati wa kujiri Vita Vikuu vya Kwabnza vya Dunia.  Na baada ya kuachiliwa huru akiwa pamoja na Wakomonisti alipigana dhidi ya utawala wa Tzar.***

Josip Tito

Na miaka 127 iliyopita, Husseinqali Hamedani, ustadhi mkubwa wa somo la akhlaqi aliaga dunia. Alizaliwa mwaka 1238 Hijria Qamaria na baada ya kumaliza masomo ya utangulizi alisoma elimu katika vitupo muhimu vya elimu na akaondokea kuwa mwalimu mahiri wa somo la akhlaqi na Irfan. Husseiniqali Hamedani alikuwa na nafasi muhimu katika uenezaji wa elimu.***

 

Kaburi la Husseinqali Hamedani 

 

Tags