Jan 21, 2018 03:12 UTC
  • Jumapili,  Januari 21, 2018

Leo ni Jumapili tarehe 3 Jamadul-Awwal mwaka 1439 Hijria sawa na tarehe 21Januari 2018 Miladia.

 

Siku kama ya leo miaka 281 iliyopita kulitokea kimbunga kikali katika Ghuba ya Bengal, mashariki mwa India na kupelekea watu laki tatu kufariki dunia. Tufani hiyo inatajwa kuwa ndiyo kubwa na iliyosababisha maafa makubwa zaidi hadi sasa katika eneo hilo. Eneo la Ghuba ya Bengal lililoko kaskazini mwa Bahari ya Hindi na kusini mwa Asia ni miongoni mwa maeneo yanayokumbwa na vimbunga na mafuriko makubwa ya mara kwa mara ambayo aghlabu husababisha hasara na maafa makubwa.

Tufani hiyo katika Ghuba ya Benghal

Siku kama ya leo miaka 225 iliyopita Mfalme Louis XIV (16) wa Ufaransa alinyongwa. Alichukua hatamu za uongozi mwaka 1774 na kuathiriwa mno na mkewe Marie-Antoinette. Mwaka 1789 wananchi wa Ufaransa walianzisha mapambano dhidi ya Mfalme Louis XIV kutokana na hali mbaya ya kiuchumi na kijamii na miaka mitatu baadaye serikali ya kifalme ikafutwa rasmi nchini Ufaransa. Hata hivyo kutokana na kuwa Mfalme Louis alikuwa ameomba msaada wa nchi za kigeni kwa siri alituhumiwa kuwa alifanya uhaini na kuhukukiwa kifo. Watu kadhaa wa familia ya Mfalme Louis XIV akiwemo mkewe Marie-Antoinette pia walinyonwa.

Mfalme Louis XIV

Siku kama ya leo miaka 147 iliyopita, alifariki dunia Ayatullah Mirza Abu Abdillah Sheikhul-Islami Zanjani, aalim na malenga aliyekuwa na uwezo mkubwa wa Waislamu. Alizaliwa mwaka 1224 Hijiria mjini Zanjan, moja ya miji ya Iran na akiwa kijana alielekea mjini Isfahan kwa ajili ya masomo. Akiwa mjini Isfahan alijiunga na chuo cha hauza ambacho kilikuwa moja ya vituo vyenye itibari katika elimu ya kidini wakati huo ambapo alifikia elimu ya juu na kisha kurejea nyumbani baada ya kuhitimu masomo yake. Sambamba na kujishughulisha na kazi ya ufundishaji Ayatullah Mirza Abu Abdillah Sheikhul-Islami Zanjani, aliandika vitabu mbalimbali ambavyo baadhi yake ni 'Hujjatul-Abraar' na 'Hidaayatul-Muttaqin'.

Ayatullah Mirza Abu Abdillah Sheikhul-Islami Zanjani

Siku kama ya leo miaka 102 iliyopita alifariki dunia Ayatullah Sayyid Ismail Swadr, alimu na mujtahidi wa ngazi ya juu mjini Kadhimiya, Iraq. Alisoma masomo ya awali ya dini ya Kiislamu kwa kaka yake na kisha akaelekea mjini Najaf, Iraq kwa ajili ya kujiendeleza zaidi katika uwanja huo. Akiwa mjini Najaf alijifunza elimu ya sheria za Kiislamu (fiqhi), elimu ya akhlaq na elimu nyingine tofauti za kidini. Baada ya kufariki dunia mwalimu wake mkubwa Ayatullah Mirza Shirazi, Ayatullah Sayyid Ismail Swadr alichukua jukumu la ufundishaji mjini Karbala nchini humo.

Sayyid Muhammad Baqir Swadir akiwa na kaka yake , Ayatullah Sayyid Ismail Swadr

Siku kama ya leo miaka 94 iliyopita, alifariki dunia Vladimir Ilyich Lenin, kiongozi wa mapinduzi ya Kikomonisti wa Urusi ya zamani. Lenin alizaliwa mwaka 1870 ambapo alianza kupambana na utawala wa kifalme wa wakati huo nchi humo tangu akiwa chuo kikuu na hadi mwaka 1900 alielekea uhamishoni nje ya nchi. Baada ya kurejea nchini alifungwa jela na wakati mwingine akabaidishwa, ambapo alikuwa akijishughulisha na kazi ya uandishi wa vitabu mbalimbali. Mwezi April 1917 alirejea Russia kwa lengo la kuongoza kwa karibu mapinduzi ya Kikomonisti nchini humo. Baada ya ushindi wa mapinduzi alikuwa kiongozi wa Urusi ya Zamani ambapo alifariki dunia katika siku kama ya leo mwaka 1924.

Vladimir Ilyich Lenin

Siku kama ya leo miaka 39 liyopita sambamba na kuanza kutetereka nguzo za utawala wa Shah nchini Iran mkabala wa wimbi kubwa la mashinikizo ya wananchi na harakati za Mapinduzi ya Kiislamu, serikali ililazimika kuwaachia huru wafungwa waliokuwa katika jela za Shah na wananchi Waislamu wa Iran wakawapokea watoto wao waliokuwa wakiteseka kwa miaka mingi katika jela hizo. Alasiri ya siku hiyo maafisa wa jeshi la anga la Iran walifanya maandamano na kutangaza uungaji mkono wao kwa harakati ya taifa la Kiislamu la Iran. Siku hiyo hiyo pia magazeti ya Iran yaliandika habari iliyokuwa na kichwa cha habari kilichosema: "Imam Khomeini Kurejea Iran Siku Kadhaa Sijazo". Habari hiyo ilizusha wimbi la hamasa na furaha kubwa kati ya wananchi wanamapinduzi wa Iran na kila mtu alianza kujitayarisha kwa ajili ya kwenda kumpokea kiongozi wa kihistoria wa Mapinduzi ya Kiislamu Imam Ruhullah Khomeini.

Harakati ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran