Mchango wa Maulamaa wa Kishia Katika Uislamu (3)+SAUTI
Assalaamu Alaykum wapenzi wasikilizaji na karibuni katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Mchango wa Maulamaa wa Kishia Katika Uislamu.
Tulisema katika kipindi chetu kilichopita kuwa, Sheikh Kulayni alikuwa alimu na msomi mkubwa zaidi wa Kishia katika karne ya tatu Hijria na alikuwa akiaminiwa na Mashia na Masuni katika kutoa fatuwa na ndio maana akaondokea kuwa mwanazuoni wa kwanza wa Kiislamu kuwa mashuhuuri kwa lakabu ya Thiqat al-Islam.
Tulieleza pia kuwa, Sheikh Kulayni alizaliwa katika zama za Imam Hassan Askary (as) na kipindi chake kusadifiana na szama za Manaibu na wawakilishi wane makhsusi wa Imam Muhammad Mahdi (atfs). Tulibainisha pia jinsi zama za Sheikh Kulayni zilivyokuwa nyeti na kujulikana kama Zama za Hadithi. Sehemu ya tatu ya mfululizo huu juma hili itaendelea kumzungumzia Sheikh Kulayni pamoja na vitabu vyake alivyoalifu. Kuweni nami hadi mwisho wa kipindi hiki.

Katika kipindi cha umri wake uliojaa baraka, Sheikh Kulayni aliandika vitabu vingi vyenye thamani kubwa, vitabu ambavyo vimekuwa dafina na turathi kubwa kwa vizazi vilivyokujaa baada yake. Miongoni mwa vitabu vyake ni: al-Rijaa, ar-Rad ala al-Qaramitah, Rasailu al-Aimah, Taabir Ru'yaa na mjumuiko wa mashairi ya kuwasifia Ahlul-Baiti (as).
Hata hivyo kitabuu muhimu na mashuhuri zaidi cha Sheikh Kulayni ni al-Kafi ambapo Sheikh Kulayni alitumia muda wa miaka 20 kukiandika. Al-Kafi ni kitabu cha kwanza miongoni mwa Kutub al-Arabaa vitabu vinne vya hadithi vyenye itibari kwa Waislamu wa Kishia. Kitabu hicho si tu kwamba, ndio kitabu muhimu na kikkubwa kkabisa cha Sheikh Kulayni, bali katika jamii ya Kiislamu na katika uwanja wa hadithi, hakuna kitabu chenye itibari kilichoalifiwa chenye itibari zaidi ya kitabu hiki.
Kitabu hiki takribani tangu karne 11 zilizopita, kimekuwa marejeo ya wana hadithi na mafakihi na nyaraka ya Mamujitahidi wakubwa wa Kishia. Katika kitabu chake cha al-Kafi, Sheikh Kulayni amekusanya humo hadithi 16,000 za Mtume (saw) na Maimamu (as). Kitabu cha al-Kafi kimegawanyika katikka sehemu tatu ambazo ni Usul, Furu'u na Raudhah. Usul al-Kafi ni mjumuiko wa maudhuui za kiitikadi na kiakhlaq. Katika sehemu hii ya kitabu hiki, Marhumu Sheikkh Kulayni amebainisha kwa uumakini na kimantiki akitumia riwaya umuhimu wa akili na nafasi yake katika kutambua maarifa.
Kisha anaelezea fadhila za kuutafuta na kkujifuunza elimu pamoja na adabuu zake. Ili kwa njia hiyo ieleweke wazi umuhimuu wa maarifa pamoja na nafasi yake katika kuthibitisha misingi ya kiitikadi. Baada ya hapo, Sheikh Kulayni anaeleza msingi muhimu zaidi wa kiitikkadi yaani Tawhihi, kumtambua na kumpwekesha Mwenyezi Mungu. Kisha katika mlango wa al-Hujja, Sheikh Kulayni amewweka humo hadithi zinazohusiana na Utume na Uimamu. Sehemu nyingine ya Usul al-Kafi inazungumzo masuala ya maadili na malezi kama: Unyenyekevu, kujizuia, kukinai, kusengenya, fadhila za dua, fadhila za Qur'ani, adabu za maingiliano na watu na kadhalika. Maudhui za mlango huu katika Usul al-Kafi zinavutia mno na ziko aina kwa aina kkwa ajili ya watu wote, yaani haihusiani na tabaka fulani la watu katika jamii.
Sehemu ya pili ya kitabu cha al-Kafi yaani 'Furu'u' inahusiana na hadithi na riwaya za masuala ya kifikihi na kisheria kama Swala, Zaka, Swaumu, Hija na kadhalika ambapo kutokana na kuwa maudhui hizo ni za kitaalamu, kikawaida wanaostafidi nazo ni wanazuoni wa fikihi. Sehemu ya tatu ya kitabu cha al-Kafi ina jina la Raudhah. Katika sehemu hii kuna hadithi 597 ambazo zinabainisha masuala mbalimbali kama khutba, barua za Maimamu, mawaidha, visa na maudhui za kihistoria ambapo ni kutokana na kuwa kwake na mauudhui mbalimbali sehemu hii ikapewa jina la Raudhah yaani bustani.
Sheikh Kulayni katikka mlango wa kwanza amejitahidi katika kitabu hiki cha al-Kafi kuweka hadithi ambazo ni sahihi zaidi na zilizo wazi zaidi na kisha baadaye akaweka hadithi ambazo haziko wadhiha na ambazo ziko katikka hali na sura ya kiujumla. Moja ya ubora wa kitabu cha al-Kafi ni kwamba, Sheikh Kulayni kila hadithi aliyonukuu amtaja sanadi ya hadithi hiyo mpaka inapoishia kwa Imam. J
Jitihada kubwa aliyoifanya Sheikh Kulayni ilikuwa ni kuhakikisha kwamba, anakusanya na kuweka humo hadithi ambazo hazipingani na Qur'ani. Kundi la Maulamaa wa Kishia linaamini kwamba, hadithi zote zilizomo kkatika kitabu cha al-Kafi ni sahihi, ilhali kuuna kundi la pili la Maulamaa wa Kishia linaloamini kwamba, katika kitabu hicho kuna hadithi ambazo ni dhaifu.
Sheikh Kulayni mwenye ameandika katika utangulizi wa kitabu cha al-Kafi kwamba: Hadithi na riwaya sahihi ambazo zinaafikiana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu.
Sheikh Mufid, alimu na mwanazuoni mkubwa mwenye daraja ya juu wa Kishia ameandika kuhusiana na kitabu cha al-Kafi: al-Kafi ni kitabu kikubwa zaidi miongoni mwa vitabu vyya Kishia na Maulamaa wetu wamenufaika na kitabu hiki kuliko kitabu kingine chochote."
Muhammad ibn Ya'qub anayejulikana zaidi kwa jina la Sheikh al‑Kulayni aliaga dunia mwaka 328 huko mjini Baghdad akiwa na umri wa miaka 70. Sheikh Kulayni aliaga dunia sambamba na kuanza kipindi cha Ghaibat al-Kubra (Ghaiba Kubwa) ya Imam Muhammad Mahdi (atsf).

Kaburi la mwanazuoni huyo mashuhuri linapatikana huko Bab al-Kufa mjini Baghdad katikka upande wa mashariki wa Mto Tigris kando ya daraja za zamani la Baghdad.
Tunakamilisha kipindi chetu hiki cha juma hili kkwa hadithi kutoka kwa Bawana Mtume (saw) ambaye amenukuliwa akisema: Luqman mwenye hekima alimwambia mwanawe: Ewe Mwanangu! Daima kkaa katika vikao vya wasomi na wanazuoni na sikiliza maneno ya wenye hekima kwani Mwenyezi Mungu huuhuisha moyyo uliokkufa kwa nuuru ya hekima; kama ambavyo huihuisha ardhi iliyokufa kwa mvua na maji.