Mar 14, 2020 02:28 UTC
  • Jumamosi, Machi 14, 2020

Leo ni Jumamosi tarehe 19 Rajab 1441 Hijria mwafaka na tarehe 14 machi 2020 Miladia.

Siku kama ya leo miaka 1432 iliyopita,  vilitokea vita vya Tabuk baina ya Waislamu na jeshi la Roma. Vita vya Tabuk ni miongoni mwa vita vya mwisho vya Mtume Muhammad (saw). Sababu ya kutokea vita hivyo ni kwamba, msafara wa kibiashara wa Sham ulimtaarifu Mtume (saw) kwamba mfalme wa Roma ametayarisha jeshi na kulituma Madina. Kwa msingi huo Mtume Muhammad (saw) aliwaamuru Waislamu kujitayarisha kwa ajili ya kukabiliana na jeshi la mfalme wa Roma. Waislamu wengi walijitayarisha kwa ajili ya vita hivyo licha ya masafa marefu, msimu wa joto kali, mashaka ya safari hiyo ngumu na kuwadia msimu wa mavuno. Hatimaye jeshi na wapiganaji elfu 30 la Waislamu liliwasili eneo la vita lakini halikukuta jeshi la mfalme wa Roma eneo hilo. Japokuwa hakukutokea mapigano wakati huo, lakini tukio hilo lilidhihirisha nguvu ya Waislamu, utayarifu wao wa kukabiliana na majeshi vamizi na moyo wao wa kujitolea kwa ajili ya Allah. Vita hivyo vya Tabuk pia vinajulikana kwa jina la "al Fadhiha" kwa maana ya mfedheheshaji kutokana na kwamba, vililifedhehesha kundi la Waislamu wanafiki waliokataa kujiunga na msafara huo kwa ajili ya kukabiliana na jeshi la Roma.***

Vita vya Tabuk

 

Miaka 967 iliyopita katika siku kama ya leo yaani tarehe 19 Rajab mwaka 474 Hijria Qamaria Abul Walid Sulaiman bin Khalaf Maliki, faqihi maarufu wa karne ya Tano Hijria Qamaria aliaga dunia huko Andalusia ambayo leo inajulikana kama Uhispania. Alikuwa hafidh na mfasiri wa Qur'ani Tukufu mbali na kubobea katika fasihi na mashairi. Abul Walid awali alifunza Fiqhi na taaluma ya Hadithi za Mtume SAW huko Andalusia na kisha akaendelea kufundisha huko Makka na Baghdad. Kati ya vitabu alivyoandika ni, "Tafsirul Qur'an", "An-Nasikhu wal-Mansukh" na Al-Isharah." ***

Abul Walid Sulaiman bin Khalaf Maliki,

 

Katika siku kama ya leo miaka 141 iliyopita alizaliwa huko Ujerumani Albert Einstein mwanafizikia na mwanahisabati hodari. Alizaliwa mwaka 1905 na baadaye akapata uraia wa Uswisi na kisha mwaka huo huo akaandika na kusambaza makala tatu ambapo moja kati ya hizo ilihusiana na msingi wa tawi jipya katika elimu ya fizikia. Mwaka 1921 kutokana na Einstein kufanya juhudi kubwa na uhakiki alifanikiwa kupata tuzo ya nobel katika taaluma ya fuzikia. ***

Albert Einstein

 

Miaka 66 iliyopita yaani mnamo mwaka 1954 tarehe 14 mwezi Machi vilianza vita vya kihistoria na vikubwa vilivyojulikana kwa jina la vita vya" Dien Bien Phu" ambavyo viliainisha mustakbali wa wanajeshi wa kikoloni wa Ufaransa huko Indochina. Katika vita hivyo wapiganaji wa harakati ya wanamapinduzi ya Viet Minh waliokuwa wakipigania ukombozi wa Vietnam walipambana na jeshi la wakoloni wa Kifaransa waliokuwa katika ngome ngumu kudhibitiwa ya Dien Bien Phu. Hatimaye tarehe 7 Mei mwaka huo huo vita hivyo vilifikia tamati kwa kusalimu amri kamanda wa majeshi ya Ufaransa aliyekuwa katika ngome ya Dien Bien Phu. Vita hivyo viliwafungisha virago wakoloni wa Ufaransa nchini Vietnam. ***

Vita vya" Dien Bien Phu

 

Katika siku kama ya leo miaka 42 iliyopita,  yaani tarehe 14 Machi 1978, jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel lilianza kuivamia na kuikalia kwa mabavu ardhi ya Lebanon kwa kisingizio cha kukabiliana na operesheni iliyofanywa na wanamapambano wa Kipalestina pambizoni mwa Tel Aviv. Katika mashambulio hayo jeshi la Israel liliua raia wengi wasio na hatia wa Lebanon na Palestina na kuikalia kwa mabavu sehemu ya ardhi ya Lebanon. Hata hivyo utawala huo ghasibu uliondoka kwa fedheha katika maeneo ya kusini mwa Lebanon mwaka 2000 baada ya kupata kipigo kikali kutoka kwa wanamapambano shupavu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah na kuondoka kwenye eneo hilo. ***

 

Miaka 40 iliyopita katika siku kama ya leo uchaguzi wa Majlisi ya kwanza ya Ushauri ya Kiislamu yaani Bunge la kwanza la Iran baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ulifanyika hapa nchini na hivyo kutimiza moja ya malengo ya mapinduzi hayo. Kwa sasa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran ina wawakilishi 290 ambao huhudumu bungeni kwa kipindi cha miaka 4. Wafuasi wa dini za waliowachache nchini Iran kama Wakristo na Wayahudi pia kwa uchache huwa na mwakilishi mmoja katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu. Bunge la Iran hutunga sheria zinazohusiana na masuala ya umma kwa sharti kwamba zisipingane na sharia za Kiislamu. Kazi nyingine muhimu ya Bunge hilo ni kuwasaili, kuwapasisha au kuwauzulu mawaziri wa serikali. ***

Uchaguzi wa Majlisi ya kwanza ya Ushauri ya Kiislamu yaani Bunge la kwanza la Iran

 

Na siku kama ya leo miaka 35 iliyopita, vibaraka wa madola ajinabi walilipua bomu katika mkusanyiko mkubwa wa wananchi wa Waislamu wa Iran katika ibada ya Swala mjini Tehran ambapo watu kadhaa waliuawa na kujeruhiwa katika jinai hiyo. Nukta ya kuzingatiwa katika mlipuko huo wa bomu katika Swala ya Ijumaa mjini Tehran ni kuwa, tukio hilo halikupelekea kusitishwa ibada hiyo ya kisiasa na kimaanawi. Ayatullah Ali Khamenei aliyekuwa Khatibu wa Swala ya Ijumaa siku hiyo aliendelea na hotuba na baada ya hapo ibada ya Swala ya Ijumaa ikafanyika kwa utulivu kamili. ***

 

Tags