Aug 13, 2021 23:55 UTC
  • Jumamosi, 14 Agosti, 2021

Leo ni Jumamosi tarehe 5 Mfunguo Nne Muharram 1443 Hijria ambayo inasadifiana na tarehe 14 Agosti 2021 Miladia.

Siku kama ya leo mika 1382 iliyopita, Abdallah bin Ziyad baada ya kutuma kikosi cha askari wengine 1000 kuelekea Karbala kwa ajili ya kupigana vita na mjukuu wa Mtume (saw) Imam Hussein (as), alimpa jukumu Bwana mmoja aliyejulikana kwa jina la Zahir ibn Qais  aliyekuwa na wapanda farasi 500 wasimame katika daraja la Sadah katika mji wa Kufa na awazuie watu wanaotaka kutoka katika mji huo na kwenda kuungana na Imam Hussein (as). Mtu aliyejuliana kwa jina la Amir bin Abi Salamah aliyekuwa ameazimia kwenda kuungana na Imam Hussein alifanikiwa kupenya. Baada yake hakuna mtu aliyethubutu kumfuata. Amir alifanikiwa kufika Karbala na kuungana na Imam Hussein (as) na akiwa huko alifanikiwa kupata daraja kubwa ya kufa shahidi. Amir alikuwa mmoja wa masahaba wa Amirul-Muuminina Ali bin Abi Twalib na alishiriki katika vita vingi akiwa pamoja na matukufu huyo. ***

 

Katika siku kama ya leo miaka 76 iliyopita yaani tarehe 14 Agosti mwaka 1945 Japan ilisalimu amri mbele ya vikosi vya Waitifaki. Kwa utaratibu huo vita vilivyokuwa vimeanza mwaka 1939 kwa mashambulizi ya Ujerumani dhidi ya Poland vikafikia kikomo. Japan na Marekani ziliingia katika vita vikali Disemba mwaka 1941. Vita hivyo vilimalizika baada ya Marekani kushambulia miji ya Hiroshima na Nagasaki kwa mabomu ya nyuklia ambayo yaliua karibu watu laki mbili. Kusalimu amri huko kwa Japan kwa hakika kulihitimisha Vita vya Pili vya Dunia. ***

Kuusalimu amri Japan katikak Vita vya Pili vya Dunia

 

Miaka 74 iliyopita katika siku ka, nchi ya Pakistan ilijitenga rasmi na India na kujitangazia uhuru wake. Dini tukufu ya Kiislamu iliingia Bara Hindi katika karne ya 8 na sehemu ya ardhi hiyo ambayo leo inajulikana kwa jina la Pakistan ilikuwa mikononi mwa Waislamu hadi wakati ilipokaliwa kwa mabavu na Waingereza mwishoni mwa karne ya 18. Chama cha Muslim League kikiongozwa na Muhammad Ali Jennah kilianzishwa mwaka 1906 kwa lengo la kuunda serikali ya Kiislamu baada ya kuanza harakati za wananchi wa India dhidi ya mkoloni Mwingereza. Chama hicho kilifanikiwa kuwashawishi Waislamu wa India na hatimaye kiliunda nchi ya Pakistan. ***

Kujitenga Pakistan na India na kujitangazia uhuru

 

Na siku kama ya leo miaka miaka 65 iliyopita yaani tarehe 14 Agosti 1954, aliaga dunia malenga na mwandishi wa Kijerumani aliyejulikana kwa jina la Bertolt Brecht. Brecht alizaliwa mwaka 1898 Miladia katika jimbo la Ugsbourg nchini Ujerumani. Malenga na mwandishi huyo wa Kijerumani alihitimu elimu ya juu katika taaluma ya sayansi asilia (bayolojia, kemia na fikikia). Malenga huyo wa Kijerumani ameacha vitabu na picha ambazo nyingi zinaeleza kuhusu utawala wa Manazi na udhalimu waliokuwa wakiutenda. ***

Bertolt Brecht.

 

Tags