Jumapili, Juni 12, 2022
Leo ni Jumapili mwezi 12 Mfunguo Pili Dhulqaad 1443 Hijria, sawa na tarehe 12 Juni 2022 Milaadia.
Tarehe 12 Juni miaka 482 iliyopita nchi ya Chile iliyoko magharibi mwa Amerika ya Kusini ilitekwa na wakoloni wa Hispania. Kabla ya hapo Wahindi Wekundu wa Chile walikuwa wamevunja hujuma na mashambulio kadhaa ya Wahispania waliokusudia kuteka na kukalia kwa mabavu ardhi yao. Hata hivyo, hata baada ya kutekwa nchi yao, Wahindi Wekundu hao waliendeleza mapambano dhidi ya wakoloni hadi pale José Francisco de San Martín jenerali wa Argentina alipowasili mwaka 1817 na kuanzisha mashambulio ya kuzikomboa nchi zote zilizokuwa chini ya ukoloni wa Hispania Kusini mwa Amerika, ikiwemo Chile. Kwa msingi huo, Chile akakombolewa na kutangaza uhuru wake mwaka 1818.
Miaka 108 iliyopita, tarehe 12 Juni 1914, kwa mara ya kwanza kabisa yalifanyika majaribio ya kutumia nishati ya joto la jua pambizoni mwa Cairo mji mkuu wa Misri. Mbunifu na mtekelezaji wa mpango huo alikuwa mwanafizikia wa Kijerumani, ambaye aliweza kukusanya miale ya jua na kufanikiwa kuwasha mashine ya mvuke yenye kutumia 'horse power' 50.
Siku kama ya leo , inayosadifiana na tarehe 12 Juni 1964, Nelson Mandela kiongozi wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini alihukumiwa kifungo cha maisha jela, baada ya kupatikana na hatia ya kufanya uhaini dhidi ya mfumo na utawala wa ubaguzi wa rangi, Apartheid nchini humo. Mandela alihukumiwa adhabu hiyo pamoja na wenzake saba akiwemo Walter Sisulu aliyekuwa Katibu Mkuu wa zamani wa chama cha African National Congress kilichokuwa kimepigwa marufuku nchini humo.
Katika siku kama ya leo miaka 99 iliyopita, Adib Neyshabouri, mshairi na malenga stadi wa Kiirani aliaga dunia. Alizaliwa mwaka 1281 Hijria Qamariakatika mji wa Neyshabur moja ya miji ya kaskazini mashariki mwa Iran. Akiwa mdogo Adib Neyshabouri alikumbwa na ugonjwa wa ndui na kuwa kipofu. Hata hivyo mapenzi yake makubwa ya kusoma na kujifunza yalimsukuma na kumfanya awe mmoja wa wasomi wakubwa hasa katika uga wa mashairi na fasihi ya lugha. Kuna beti takribani 6,000 za mashairi ya msomi huyo zilizokusanywa hadi sasa.***
Siku kama ya leo miaka 31 iliyopita inayosadifiana na 12 Juni 1991, ulifanyika uchaguzi wa kwanza wa Rais wa Shirikisho la Russia. Baada ya kusambaratika Urusi ya zamani, Russia kama zilivyokuwa nchi nyingine zilizokuwa zikiunda Umoja wa Kisovieti zilijipatia uhuru wake. Boris Yeltsin aliiongoza nchi hiyo kwa vipindi viwili, hadi mwezi Disemba 1999, alipoamua kung'atuka madarakani.
Siku kama ya leo miaka 43 iliyopita inayosadifiana na tarehe 12 Juni 1975, Indira Gandhi Waziri Mkuu wa wakati huo wa India alizuiwa kuendelea na wadhifa huo kwa miaka sita, baada ya kupatikana na hatia ya kufanya udanganyifu katika uchaguzi. Hata hivyo Indira Gandhi alipinga miito iliyomtaka ajiuzulu na akatangaza mipango ya kukata rufaa katika mahakama kuu ya India. Siku kama ya leo miaka 470 iliyopita, ardhi ya Chile huko magharibi mwa Amerika ya Kusini ilivamiwa na wakoloni wa Kihispania. Kabla ya uvamizi huo, Wahindi Wekundu wa Chile waliushinda uvamizi wa Uhispania uliokuwa na lengo la kuikalia kwa mabavu ardhi yao.