Mar 12, 2023 07:34 UTC
  • Hakika ya Uwahabi 11

Tulisema katika kipindi kilichopita kwamba Mawahabi hujiita kuwa ni Masalafi yaani wafuasi wa watu wema waliotangulia. Katika kipindi cha leo tutachambua kwa undaji kidogo maana halisi ya neno 'Salaf' ili tupate kujua maana halisi ya 'Salaf Swaleh' na maana inayokusudiwa na Mawahabi.

Bismillahi Rahmanir Raheem. Tunaanza kwa jina la Mwenyezi Mungu ambaye alimtuma Mtume wake Mtukufu (saw) ili awe rehema kwa walimwengu na kumpa sifa zote njema ili kumuusia aweze kuongoza na kuzungumza na waja wake kwa njia bora na ya busara.

Salamu za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya wasikilizaji wetu ambao hutusikilizaji kila siku na wale wote ambao ni mara yao ya kwanza kujiunga nasi katika kipindi hiki, karibuni.

Tulisema katika kipindi kilichopita kwamba Mawahabi hujiita kuwa ni Masalafi yaani wafuasi wa watu wema waliotangulia. Katika kipindi cha leo tutachambua kwa undaji kidogo maana halisi ya neno 'Salaf' ili tupate kujua maana halisi ya 'Salaf Swaleh' na maana inayokusudiwa na Mawahabi.

*************

Maana ya 'salaf' au 'aslaaf' ni watu wa zamani au kwa ibara nyingine waliotutangulia. Kinyume chake ni 'khalaf' au 'aklaaf' yaani waliokuja baadaye kwa lugha ya Kiarabu. Hii ni ndio maana jumla ya maneno hayo. Maneno hayo yanakumuisha sehemu na zama zote. kwa maana kuwa kila mtu katika zama anazoishi ni 'khalaf' wa waliopita na ni 'salaf' wa watakaokuja baada yake. Kutokana na ukweli kuwa Waislamu wote wanataka kumfuatya Mtume Mtukufu (saw) pamoja na wafuasi wake waaminifu na wenye imani, tunaweza kusema kuwa Waislamu wote bila kujali madhehebu zao ni Masalafi kwa njia moja au nyingine. Lakini maana ya kiistalahi ya neno 'Salaf Swaleh' ambayo takriban ilianza kuenezwa katika jamii ya Kiislamu katika karne ya nane Hijria kutokana na fikra za Ibn Taymiyya, wanakusudiwa watu na shakhsia ambao waliishi katika karne tatu za mwanzo wa historia ya Uislamu, yaani Mtume Mtukufu (saw), Masahaba na wafuasi wa masahaba hao au kwa jina mashuhuri Tabieen, na pia wafuasi wa Tabieen.

Kwa kuzingatia ufahamu potofu aliokuwa nao kuhusiana na Aya za Qur'ani na Hadithi za Kiislamu, Ibn Taymiyya alianzisha mkondo potofu wa itikadi za Kislamu ambao baadaye uliendelezwa na wanafunzi wake. Upinzani mkali dhidi ya matumizi na hoja za kiakili, falsafa na mantiki, hoja za kiitikadi (kalaam), kuendesha vita dhidi ya waliobobea katika elimu hiyo, kushajiisha kufuata Hadithi bila kuzihoji na kukufurisha Waislamu wa madhehebu nyingine za Kiislamu ni baadhi ya itikadi muhimu zinazoenezwa na Mawahabi katika zama hizi.

Mawahabi

************

Kwa hoja ya kurejea katika utamaduni na nyendo za waliotangulia, Mawahabi wanadai kuwa kila mtu anapasa kurejea mwenyewe katika maandiko ya Qur'ani Tukufu na kufahamu mwenye yaliyoandikwa humo kwa sababu kwa mujibu wa mtazamo, lililo na umuhimu ni lugha ya Kiarabu na kwa hivyo mtu anapokua kusoma na kufahamu lugha ya Kiarabu anaweza kujijazia mwenyewe maana ya maneno na ibara zilizonadikwa katika kitabu hicho cha mbinguni. Kwa mtazamo wa Mawahabi ufahamu wa kidhahiri wa kila mtu kutokana a Aya na Hadithi za Kiislamu unamuwezesha kufanyia kazi aliyoyafahamu kwenye maandiko hayo na kwamba hivyo ndivyo unavyotaka Uislamu. Kwa kuwa ni itkadi kama hiyo, kwanza Mawahabi huwa wamefutilia mbali msingi muhimu wa 'taqlidi' ambo ni kufuata wanazuoni waliobeobea katika sheria za dini, na pili huwa wameandaa uwanja wa kudhihiri fujo na mparaganyiko katika jamii ya Kiislamu kuhusiana  na masuala ya sheria na itikadi. Kwa maneno mengine ni kuwa Mawahaabi wanadai kuwa Aya za Qurlani hazina maana nyingine ya batini na iliyofichika ambayo haiwezi kufahamika ila na wenye ujuzi na waliobobea kwenye maana hizo na kuwa kila mtu ana uwezo wa kufahamu na kudiriki vyema Aya na Hadithi za Kiislamu bila kuhitajia msaada wa wanazuoni na wajuzi wa mambo. Jambo linalosisitizwa na Mawahabi ni kuzingatia dhahiri ya Aya na Hadithi tu bila kuzichambua kwa undani. Kidhahiri Mawahabi hawahawahi kusikia au hawayapi umuhimu maneno ya Mtume Mtukufu (saw) yanayosema: 'Qurani ina dhahiri na batini, na batini hiyo bado ina batini nyingine hadi batini saba.' Baadhi ya wataalamu wa Hadithi hata wamezitaja batini hizo kuwa ni sabini.

Makhawarij mambo leo

Misimamo ya Mawahabi kuhusiana na Qur'ani tukufu inatukumbusha kundi jingine lililodhihiri mwanzoni mwa Uislamu ambalo nara yao kubwa ilikuwa ni: 'La Hukma Ila Lillah' yaani hukumu (uongozi/utawala) ni ya Mwenyezi Mungu pekee...Nam kundi hilo ni la Makhawarij. Kundi hilo lilikuwa likidai kuwa baada ya kuaga dunia Mtume Mtukufu (saw) hakuna mtu mwingine ambaye alikuwa na haki ya kuongoza na kutawala jamii ya Kiislamu. walikuwa wakipinga vikali umar'ja na kujichukulia kuwa wao tu ndio waliokuwa na ufahamu sahihi wa Uislamu na wakuwachukulia Waislamu wengine kuwa wasiojua lolote katika dini. Mnakumbuka vuziri wasikilizaji wapenzi kuwa tuliwahi kusema katika moja ya vipindi vilivyopita kwamba Mawahabi wanafanana sana kifikra na Makhawarij. Makundi mawili hayo yanafanana sana kuhusiana na tabia ya kuwakufurisha Waislamu, katika taasubi, ghasia na utumiaji mabavu katika kuhalalisha mitazamo na itikadi zao. Sasa tunaweza kufahamu vizuri makusudio ya Mawahabi wanapozungumzia ibara ya 'Salaf Swaleh.'

************

Kabla ya Waislamu kutambua na kuwazingatia Makhawarij kihistoria, wanatambua na kuzingatia sunna, sira na nyendo za maisha ya Mtume Mtukufu (saw), Maimau na wafuasi wao wema. Sote tunajua vizuri kwamba katika vita, Mtume (saw) daima alikuwa akiwausia wafuasi wake kuzingatia haki za watu. Alikuwa akiwapa makamanda wake amri ya moja kwa moja kwa kuwaambia: 'Msifanye hiana, msivunjia heshima maiti, msikiuke mikataba na wala msiwaue wazee, watoto na wanawake.' Mtume wa Mwewnyezi Mungu (saw) hata aliwakataza wapiganaji na wafuasi wake kuwaua waliojitenga na dunia, watawa na wajumbe wa maadui. Mtume Muhammad aliwatahadharisha vikali wafuasi wake dhidi ya kuchafua kwa sumu miji ya washirikina na makafiri kwenye vita.

Mtume (saw) alikuwa akiamiliana kiutu na vizuri sana na maadui, jambo linaloonekana wazi katika ukombozi wa mji mtakatifu wa Makka. Katika hali ambayo washirikina wa Makka waliudhi na kumtesa sana walipokuwa madarakani na hatimaye kumfukuza katika mji huo baada ya kumfanyika kila aina ya udhia ikiwa ni pamoja kuendesha vita kadhaa dhidi yake na kuua jamaa na masahaba zake wa karibu zaidi na vile vile kuwajeruhi wengine wengi, lakini baada ya kuikomboa Makka, Mtume (saw) aliwasamehe wote na kuwaachilia huru.

Alikuwa akiamiliana vyema mno na wafungwa na pia akiwausia wengine waamiliane nao kiutu na wajiepushe kuwatesa. Ni vipi Mtume aliye ni huruma, rehema na utu wa kiwango jiki ambaye aliwaachilia huru wafungwa makafiri na washirikina elfu sita bila ya kuwatoza gharama wala fidia yoyote na hata kuwaombea maghfira kutoka kwa Mwewnyezi Mungu, atahusishwa hata kwa chembe na makatili ambao wanahalalisha damu, mali na heshima ya Waislamu?!! Hapana!...Hapana!! Hili haliwezekani kabisa! Kwa uchache kwetu sisi ambao tumelelewa na kuufahamu vizuri Uislamu na maisha ya Mtume Mtukufu pamoja na Watu wema wa Nyumba yake tukufu (saw).

**********

Katika dunia ya leo istilahi ya neno 'Usalafi' umepata maana mpya zaidi miongoni mwa Waislamu wa madhehebu ya Suni. Maana hii inahusishwa na kipindi cha mwamko katika katika zama hizo na inakusudiwa watu ambao wanafanya juhudi za kuwaepusha Waislamu na fikra potofu za nchi za Magharibi. Watu hao ni wale ambao wameazimia kuwarejesha Waislamu katika utamaduni na ustaarabu halisi wa Kiislamu na kuzingatia mafundisho ya Qur'ani na sunna za Mtume (saw). Waislamu hao wa Kisalafi, kinyume na walivyo Mawahabi ambao hupinga kila nembo ya teknolojia na ustaarabu mpya, wana nia nzuri ya kutazama upya fikra nzuri ya elimu na teknolojia ya kisasa kwa ajili ya kuuhudumia umma wa Kiislamu. Kusidio la kundi hilo kuhusu usalafi, ni kuondoa kutu na uchafu wote ambao umeufunika usafi na mng'aro wa Uislamu na hatimaye kuitenga dini hii tukufu na bida' pamoja na itikadi zisizo na msingi ili dini hii iweze kurejesha hadhi na hafasi yake bora ya kuwa ni dini ya kazi, jitihada na maisha yenye uchangamfu na furaha.

Bendera ya Masalafi wa zama hizi (Ikhwanul Muslimeen)