Wakimbizi wa kambi ya Dadaab waanza kurejeshwa makwao
Operesheni ya kuwarejesha makwao wakimbizi wanaoishi katika kambi ya Dadaab huko mashariki mwa Kenya imeanza kutekelezwa.
Ripoti zinasema kundi la kwanza la wakimbizi wa kambi ya Dadaab ambao wengi wao ni raia wa Somalia, lilianza kurejeshwa makwao jana Ijumaa.
Imepangwa kuwa kambi hiyo ambayo inahesabiwa kuwa kubwa zaidi ya wakimbizi dunia, itakuwa imefungwa kikamilifu hadi kufikia mwezi Mei mwaka 2017.
Kwa miezi sasa serikali ya Kenya imekuwa ikifanya jitihada kubwa za kuhakikisha wakimbizi hao wanarejeshwa makwao.
Siku hache zilizopita kamati inayoshughulikia wakimbizi wanaoishi katika kambi ya Dadaab nchini Kenya ilitangaza kuwa, nusu ya wakimbizi hao watarejeshwa nchini kwao ifikapo mwishoni mwa mwaka huu wa 2016.
Maelfu ya wakimbizi hususan kutoka nchi jirani ya Somalia wanaishi katika kambi hiyo.