Apr 09, 2024 07:57 UTC
  • Francei Molloy
    Francei Molloy

Balozi wa Afrika Kusini nchini Iran amesema kuwa jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel huko Ukanda wa Gaza ni mauaji ya kimbari.

Serikali ya Afrika Kusini ambayo ni mtetezi mkubwa wa wananchi wa Palestina na mkosoaji wa Israel katika mauaji ya kimbari ya hivi sasa ya utawala huo ghasibu katika Ukanda wa Gaza, imewaburuza viongozi wa utawala huo katika Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ) kwa  jinai za kivita na kukiuka wa Mkataba wa Geneva wa mwaka 1948 unaopiga marufuku mauaji ya kimbari. 

Afrika Kusini katika mahakama ya ICJ dhidi ya Israel 

Shirika la Habari la Iran (IRNA) limeripoti kuwa  Francei Molloy, balozi wa Afrika Kusini nchini Iran, ameeleza kuwa Afrika Kusini ikiwa nchi huru na mwanachama wa Umoja wa Mataifa inataka utawala wa Kizayuni uhukumiwe ili kuhitimisha mauaji ya kimbari ya utawala wa huo.   

Molloy aidha amekumbusha uhusiano wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Afrika Kusini uliotokana na historia ya mapambano ya ukombozi wa Afrika Kusini na kusema: Uhusiano huu hadi sasa umekuwa na manufaa kwa nchi mbili.  

Mwanadiplomasia huyo wa Afrika Kusini ameongeza kuwa: Iran ni nchi muhimu na yenye taathira katika Asia ya Magharibi na miongoni mwa nchi kubwa za Kiislamu na kwamba  Jumuiya ya  Nchi za Kiislamu imeyaleta pamoja mataifa ya Kiislamu na Iran ina nafasi muhimu sana miongoni mwa nchi hizo.

Tags