Apr 18, 2024 04:37 UTC
  • Rais wa Zambia: Tunahitaji karibu dola bilioni moja kwa ajili ya misaada ya kibinadamu

Rais wa Zambia amesemam kuwa nchi yake inahitaji haraka Kwacha bilioni 23.5 sawa na dola milioni 937 ili kukidhi mahitaji ya haraka ya kuokoa maisha na kudhamini misaada ya kibinaamu kufuatia ukame mkubwa unaoikumba nchi hiyo.

Rais Hichelema amesema kuwa kwa moyo mkunjufu na kwa niaba ya serikali na wananchi wa Zambia, anatoa wito kwa jamii ya kimataifa, washirika wa nchi hiyo, na sekta binafsi kuiunga mkono kifedha nchi hiyo ili kupunguza madhara makubwa ya ukame.

Zambia yaathiriwa na ukame mkubwa 

Rais wa Zambia pia ameeleza kuwa mwaka huu nchi hiyo imepata mvua za kiwango cha chini na hivyo kusababisha ukame mkubwa nchini. Amesema, athari za ukame zimeshuhudiwa waziwazi katika mavuno ya mazao ya kilimo; ambapo hekta milioni moja za mahindi yaliyopandwa zimeathirika vibaya katika wilaya 84 kati ya 116 za huko Zambia. 

Takriban watu milioni 9.8 wameathiriwa vibaya na ukame nchini Zambia, huku milioni 6.6 wakihitaji msaada wa haraka wa kibinadamu. Rais Hakainde Hichelema ameongeza kuwa anaamini pakubwa kwamba washirika mbalimbali wa ndani na kimataifa wataungana na serikali yake na wananchi wa Zambia ili kupunguza hali mbaya ya kibinadamu na athari nyingine mbaya za ukame unaoikumba nchi hiyo.

 

Tags