Juba yapinga kutumwa wanajeshi wa kulinda amani katika mipaka ya Sudan mbili
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i12364-juba_yapinga_kutumwa_wanajeshi_wa_kulinda_amani_katika_mipaka_ya_sudan_mbili
Sudan Kusini imesisitiza kuwa kikosi cha kulinda amani cha Kiafrika hakiwezi kutumwa katika mipaka ya pamoja ya nchi hiyo na Sudan.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 31, 2016 23:28 UTC
  • Juba yapinga kutumwa wanajeshi wa kulinda amani  katika mipaka ya Sudan mbili

Sudan Kusini imesisitiza kuwa kikosi cha kulinda amani cha Kiafrika hakiwezi kutumwa katika mipaka ya pamoja ya nchi hiyo na Sudan.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan Kusini ilitoa taarifa  jana Jumapili na kubainisha kuwa kikosi cha kulinda amani cha Kiafrika kinaweza kutumwa katika maeneo matatu tu yaani huko Juba, Bor na Bentiu nchini humo  na kwamba kikosi hicho hakiruhusiwi kuwepo katika mipaka ya pamoja ya nchi mbili za Sudan na Sudan Kusini. 

Huko nyuma kiongozi mmoja wa Sudan alidokeza kuwa wanajeshi wa kulinda amani wa Kiafrika zaidi ya elfu kumi wanatazamiwa kutumwa katika mipaka ya pamoja ya nchi mbili hizo.

Askari jeshi wa kulinda amani wa AU

Hii ni katika hali ambayo hali ya kibinadamu huko Sudan Kusini ingali inatia wasiwasi, licha ya kuwepo wawakilishi wa taasisi za kimataifa nchini humo. Mapigano makali yaliyojiri Juba mwanzoni mwa mwezi huu wa Julai kati ya vikosi vya serikali na wanamgambo watiifu kwa Riek Machar yalisababisha kuuliwa watu zaidi ya 300.