Wanafunzi wa chuo cha polisi watimuliwa Misri, kisa wana uhusiano na Ikhwani
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i1303-wanafunzi_wa_chuo_cha_polisi_watimuliwa_misri_kisa_wana_uhusiano_na_ikhwani
Serikali ya Misri imewatimua shule makumi ya wanafunzi wa Chuo cha Poilisi ya nchi hiyo kwa tuhuma ya kuwa na uhusiano na kundi la Ikhwanul Muslimin.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 15, 2016 11:43 UTC
  • vikosi vya usalama Misri
    vikosi vya usalama Misri

Serikali ya Misri imewatimua shule makumi ya wanafunzi wa Chuo cha Poilisi ya nchi hiyo kwa tuhuma ya kuwa na uhusiano na kundi la Ikhwanul Muslimin.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Misri, Meja Jenerali Amru al A'sar ambaye pia ni mkuu wa Chuo cha Polisi ya nchi hiyo amesema kuwa, chuo hicho kimewafukuza wanafunzi 40 kwa sababu ya kuwa na mfungamano na Ikhwanul Muslimin.

Misri imekuwa ikishuhudia ukandamizaji mkubwa wa wanachama wa harakati ya Ikhwanul Muslimin tangu baada ya kupinduliwa rais halali wa nchi hiyo, Muhammad Morsi mwaka 2013. Mamia ya wanachama na viongozi waandamizi wa harakati hiyo wamehukumiwa kifo na maelfu ya wengine kufungwa jela.

Jumuiya nyingi za kutetea haki za binadamu za kimataifa zinasema kuwa serikali ya Rais wa sasa wa Misri, Jenerali Abdul Fattah al Sisi inawakandamiza zaidi wapinzani wake kuliko kipindi cha utawala wa dikteta wa zamani wa nchi hiyo, Hosni Mubarak.