Sudan Kusini yailalamikia Congo DR kwa kushiriki kumtoa Juba Riek Machar
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i14104-sudan_kusini_yailalamikia_congo_dr_kwa_kushiriki_kumtoa_juba_riek_machar
Serikali ya Sudan Kusini imeilalamikia rasmi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa kile ilichokitaja kuwa kushiriki nchi hiyo kumtoa mjini Juba na kumsafirisha Riek Machar hasimu wa kisiasa wa Rais Salva Kiir.
(last modified 2026-03-03T12:46:59+00:00 )
Aug 27, 2016 23:56 UTC
  • Sudan Kusini yailalamikia Congo DR kwa kushiriki kumtoa Juba Riek Machar

Serikali ya Sudan Kusini imeilalamikia rasmi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa kile ilichokitaja kuwa kushiriki nchi hiyo kumtoa mjini Juba na kumsafirisha Riek Machar hasimu wa kisiasa wa Rais Salva Kiir.

Mawen Makol, msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Sudan Kusini ametangaza kuwa, serikali yua Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilituma helikopta kadhaa mjini Juba kwa ajili ya kumtoa mjini humo Riek Machar.

Makol amesema kuwa, serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilifanya hivyo bila kuijulisha serikali ya Juba suala ambalo ni kiyume kabisa na utaratibu na hivyo kukiuka anga ya nchi hiyo. 

Askari wa MONUSCO

Amesema, Sudan Kusini imemtaka balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mjini jibu atoe maelezo kuhusiana na kuingia huko Congo Riek Machar. Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Sudan Kusini amesema kuwa, Juba inasubiri majibu ya viongozi wa Kinshasa kuhusiana na suala hilo.

Wakati huo huo balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huko Sudan Kusini amesema kuwa, ataelekea Kinshasa kwa ajili ya mashauriano na viongozi wa serikali na wa Umoja wa Mataifa na kisha kutoa ripoti kuhusiana na jinsi Machar alivyoondoka Juba na kuibuka katika Jamhuri ya KIdemokrasia ya Congo. 

Wakimbizi wa Sudan Kusini

Hivi karibuni viongozi wa Jamhri ya Kidemokrasia ya Congo walinukuliwa wakisema kwamba, walikiagiza kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini humo (MONUSCO) kisaidie kumhamisha Machar na familia yake kutoka sehemu moja karibu na mpaka wa Sudan Kusini na kumpeleka katika eneo salama. umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, kikosi cha MONUSCO hakikuhusika katika kumondoka Riek Machar huko Sudan Kusini.