Sudan Kusini yakosoa kutoroshwa nchini humo Riek Machar
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i14206-sudan_kusini_yakosoa_kutoroshwa_nchini_humo_riek_machar
Waziri wa Habari wa Sudan Kusini ameeleza kuwa hatua ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ya kufanikisha kuondoka Juba Riek Machar Makamu wa zamani wa Rais wa Sudan Kusini ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 29, 2016 09:46 UTC
  • Sudan Kusini yakosoa kutoroshwa nchini humo  Riek Machar

Waziri wa Habari wa Sudan Kusini ameeleza kuwa hatua ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ya kufanikisha kuondoka Juba Riek Machar Makamu wa zamani wa Rais wa Sudan Kusini ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa.

Michael Makuei Lueth amesiistiza kuwa kitendo cha kumsafirisha kinyume cha sheria Riek Machar na kufanikisha kuondoka huko Sudan Kusini kulikofanywa na Kongo, ni ukiukaji wa wazi wa anga ya Sudan Kusini. Kueth amesema kuwa, hatua hiyo ya Kongo ni kinyume na sheria za kimataifa na kwamba matokeo yake yatakuwa ni kuitumbukiza hatarini amani, uthabiti na usalama wa maeneo ya mpakani na hata eneo zima kwa ujumla.

Kuhusiana na suala hilo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan Kusini pia imemuita Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo huko Juba na kumbainisha malalamiko ya nchi hiyo kuhusu hatua ya nchi yake ya kumsafirisha Machar kinyume cha sheria na kukiuka anga ya Sudan Kusini. Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan Kusini imeongeza kuwa viongozi wa Kongo wanapasa kujibu hatua yao hiyo iliyo kinyume na sheria za kimataifa. Wizara ya Mambo ya Nje ya Kongo inatazamiwa kuwasilisha ripoti kuhusu namna Machar alivyooondoka huko Juba kwa viongozi wa Sudan Kusini.

Riek Machar Makamu wa zamani wa Rais wa S/Kusini aliye katika nchi jirani ya Sudan