Sep 18, 2016 06:57 UTC
  • Mapigano kati ya pande zilizosaini makubaliano ya amani Mali

Watu 10 wameuawa katika mapigano kati ya pande zilizosaini makubaliano ya amani huko Mali.

Mapigano kati ya kundi lenye silaha linaloiunga mkono serikali ya Mali kwa jina Gatia na kundi la pili la Harakati ya UKombozi ya Azawad (CMA) yamepigana katika eneo la Intachdayte umbali wa kilomita 85 kaskazini mashariki mwa mji wa Kidal kaskazini mwa Mali. Almou Ag Mohamed msemaji wa kundi la CMA amesema kuwa wapiganaji wao sita wameuawa kwenye mapigano hayo na mmoja hajulikani alipo.  

Wapiganaji wa harakati ya Gatia wa huko Mali

Mohamed Ag Telouf mmoja wa wawakilishi wa kundi lenye silaha la Gatia amesisitiza kuwa ngome moja ya Harakati ya ukombozi ya Azawad inayosimamiwa na Kamanda Mohamed Najim imeshambuliwa. Harakati ya Ukombozi ya Azawad imesisitiza katika taarifa yao kuwa Harakati ya Gatia ndiyo iliyotekeleza shambulio hilo kwenye ngome yao.  Harakati ya Ukombozi ya Azawad imekosoa hatua ya Harakati ya Gatia ya kukiuka makubaliano ya usitishaji vita  na kutahadharisha kuwa Harakati ya Azawad haiwezi kupuuza mashambulizi ya makundi ambayo yanapatiwa silaha na zana za kijeshi na jeshi la Mali. 

Tags