Sudan inawahifadhi wakimbizi wa S/Kusini karibu laki nne
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i15814-sudan_inawahifadhi_wakimbizi_wa_s_kusini_karibu_laki_nne
Sudan imetangaza kuwa inawahifadhi wakimbizi wa Sudan Kusini karibu laki nne ambao wamelazimika kuikimbia nchi yao kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
Sep 22, 2016 00:48 UTC
  • Sudan inawahifadhi wakimbizi wa S/Kusini karibu laki nne

Sudan imetangaza kuwa inawahifadhi wakimbizi wa Sudan Kusini karibu laki nne ambao wamelazimika kuikimbia nchi yao kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Babakar Dinga Waziri wa Mambo ya Ndani wa Sudan amesema maafisa wa nchi hiyo wamewasajili jumla ya wakimbizi laki nne wa Sudan Kusini. Ameongeza kuwa wakimbizi wa Sudan Kusini wanaendelea kuwasili nchini Sudan. Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) pia Ijumaa iliyopita lilitangaza kuwa idadi ya wakimbizi wa Sudan Kusini imepindukia milioni moja. Umoja wa Mataifa pia umetangaza kuwa idadi ya wakimbizi wa Sudan Kusini waliopo nchini Sudan hadi tarehe 31 mwezi Agosti mwaka huu iliongezeka na kufikia 247,000; ambapo wakimbizi elfu 90 kati yao waliwasili Sudan tangu mwezi Januari mwaka huu.

Raia wa Sudan Kusini wakiondoka nchini na kuelekea katika nchi jirani

Uganda, Ethiopia, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Afrika ya Kati na vile vile baadhi ya nchi nyingine zimewapokea makumi ya maelfu ya wakimbizi kutoka  Sudan Kusini.