Sep 26, 2016 04:39 UTC
  • Mwanasiasa: Uchochezi wa Saudia Nigeria, ndio chanzo cha kushambuliwa Mashia

Mtaalamu mashuhuri wa masuala ya kisiasa nchini Nigeria amesema kuwa, upenyaji wa utawala wa Aal-Saud nchini humo, ndio chanzo cha kushambuliwa Waislamu wa Kishia.

Abayomi Azikiwe, mhariri wa mtandao wa habari wa Pan-African ameyasema hayo katika mahojiano na kanali ya televisheni ya Press TV ambapo sanjari na kuashiria hali mbaya kiafya ya Sheikh Ibrahim Yaqoub El Zakzaky, kiongozi wa harakati ya Kiislamu ya Nigeria ambaye hadi sasa anaendelea kushikiliwa na vyombo vya serikali ya nchi hiyo amesema kuwa, machafuko yanayoshuhudiwa Nigeria yanatokana na upenyaji wa Saudia ndani ya taifa hilo.

Maandamano ya Waislamu wa Nigeria wakitaka kuachiliwa huru sheikh Zakzaky

Amesisitiza kuwa, khofu na wasi wasi mkubwa uliowapata watawala wa Saudia ilikuja kutokana na ongezeko la kila siku la idadi kubwa ya Waislamu wa Kishia nchini humo na kwamba kitendo cha Aal-Saud kumuhonga fedha za mafuta Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria, ndicho kulichopelekea kujiri jinai za kutisha dhidi ya Waislamu wa Kishia wa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika. Hii ni katika hali ambayo, Alkhamis iliyopita, maelfu ya Waislamu nchini Nigeria walifanya maandamano makubwa mjini Abuja wakitaka kuachiliwa huru Sheikh Ibrahim El Zakzaky, mke wake na Waislamu wengine waliotiwa nguvuni tangu mwaka uliopita. Hata hivyo maandamano hayo ya amani, yalikabiliwa na mtutu wa bunduki kutoka kwa polisi ya Nigeria, huku baadhi ya Waislamu wakitiwa mbaroni.

Husseiniya ya Waislamu baada ya kubomolewa na jeshi katili la Nigeria

Itakumbukwa kuwa, tarehe 13 mwezi Disemba mwaka jana, jeshi la Nigeria lilishambulia Husseiniyyah na makazi ya Sheikh Zakzaky katika mji wa Zaria na kutekeleza jinai ya kutisha dhidi ya Waislamu wanaokadiriwa 1000 na kwenda kuwazika katika kaburi moja mjini hapo, kitendo kilichokosolewa vikali na asasi mbalimbali za ndani na nje ya Nigeria na kuwataka wahusika wake watiwe mbaroni.

Rais Buhari akiwa na Salman bin Abdulaziz Al Saud, Mfalme wa Saudia

 

Tags