Sudan yaunga mkono kutumwa wanajeshi wa Kiafrika nchini Sudan Kusini
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i16228-sudan_yaunga_mkono_kutumwa_wanajeshi_wa_kiafrika_nchini_sudan_kusini
Serikali ya Sudan imesema kuwa inaunga mkono kutumwa wanajeshi wa kulinda amani wa Kiafrika huko Sudan Kusini.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Sep 28, 2016 03:39 UTC
  • Sudan yaunga mkono kutumwa wanajeshi wa Kiafrika nchini Sudan Kusini

Serikali ya Sudan imesema kuwa inaunga mkono kutumwa wanajeshi wa kulinda amani wa Kiafrika huko Sudan Kusini.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan  imeeleza kuwa ipo tayari kushirikiana na Jumuiya ya Kieneo ya IGAD ili kurejesha amani na uthabiti huko Sudan Kusini. 

Serikali ya Sudan imetaka kutumwa haraka  askari jeshi wa kulinda amani wa Kiafrika katika kalibu ya kikosi cha Umoja wa Mataifa huko Sudan Kusini kwa lengo la kuzuia hatua yoyote ya kijeshi  na kushtadi mzozo wa ndani nchini humo.  

Raia wa Sudan Kusini waliolazimika kuwa wakimbizi kutokana na mzozo wa nchi hiyo 

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imeeleza kuwa, amani na uthabiti wa Sudan unahusiana kikamilifu na Sudan Kusini na kuzitolea wito pande zinazozozana nchini humo kutekeleza makubaliano ya amani. Serikali ya Sudan Kusini hivi karibuni iliafiki kutumwa nchini humo wanajeshi elfu nne wa Kiafrika baada ya Umoja wa Mataifa kuwasilisha azimio katika uwanja huo, na wakati huo huo imechukua  pia misimamo tata na isiyofahamika.