Wafungwa wa kisiasa 2500 wagoma kula huko Misri
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i16594-wafungwa_wa_kisiasa_2500_wagoma_kula_huko_misri
Wafungwa 2500 wa kisiasa nchini Misri wamegoma kula chakula na dawa wakilalamikia hali mbaya katika jela walipofungwa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 03, 2016 10:29 UTC
  • Wafungwa wa kisiasa 2500 wagoma kula huko Misri

Wafungwa 2500 wa kisiasa nchini Misri wamegoma kula chakula na dawa wakilalamikia hali mbaya katika jela walipofungwa.

Wafungwa hao wa kisiasa waliofungwa katika magereza ya Cairo mji mkuu wa Misri wamegoma kula chakula na dawa wakipunga vitendo vya dhulma na vizuizi vikali wanavyowekewa na maafisa husika wa jela hiyo. Aghalabu ya wafungwa wa kisiasa waliopo katika jela ya Tora mjimi Cairo wameanza kugoma kula chakula na dawa wakilalamikia mwenendo mbaya wa mafisa husika wa jela hilo.

Jelal ya Tora iliyoko Cairo, Misri inavyoonekana kwa mbele

Kundi jingine la wafungwa pia leo limeanza mgomo  wa kutokula chakula wakilalamikia vitendo vya kichochezi vya mkuu wa jela na ukatili wanaofanyiwa wafungwa hao wakati wa kuonana na familia zao. Miongoni mwa dhuma wanazofanyiwa wafungwa hao wa kisiasa wa Jela ya Tora ya Cairo ni kuzuiwa idadi kubwa ya wafungwa kuonana na ndugu zao kwa muda wa mwezi mmoja na pia kuondolewa vibali vya kuonana na familia zao katika siku za kawaida na za dharura.

Wafungwa wa kisiasa 2500 wamegoma kula chakula na dawa nchini Misri