UN: $3 billioni zahitajika kuinusuru Jamhuri ya Afrika ya Kati
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i19684-un_3_billioni_zahitajika_kuinusuru_jamhuri_ya_afrika_ya_kati
Dola takribani bilioni tatu zinahitajika ili kuisaidia Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, kujikwamua baada ya miaka kadhaa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyopeleka maelfu ya watu kuwa wakimbizi na kuliacha taifa hilo njia panda kiuchumi, kiusalama na kimaendeleo.
(last modified 2026-03-27T07:58:19+00:00 )
Nov 18, 2016 00:23 UTC
  • UN: $3 billioni zahitajika  kuinusuru Jamhuri ya Afrika ya Kati

Dola takribani bilioni tatu zinahitajika ili kuisaidia Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, kujikwamua baada ya miaka kadhaa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyopeleka maelfu ya watu kuwa wakimbizi na kuliacha taifa hilo njia panda kiuchumi, kiusalama na kimaendeleo.

Hayo ni kwa mujibu wa naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson anayehudhuria mkutano maalumu wa kuchangisha fedha kwa ajili ya CAR mjini Brussel Ubelgiji. Mkutano huo unajumuisha wahisani kutoka nchi za Umoja wa Ulaya, Bank ya Dunia na Umoja wa Mataifa. Eliasson ameongeza kuwa,  mkutano huo uliofanyika Alhamisi utasaidia nchi hiyo kisiasa ,kuleta amani na kutoa mwelekeo wa muafaka, maridhiano na maendeleo. Amesema watu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati  wanahitaji ahadi ya muda mrefu na msaada. Kikao hicho cha Brussels kimefanikiwa kupata ahadi ya misaada ya $ billioni mbili kutoka kwa wafadhili wa kimataifa.

Kwa upande wake, Rais wa CAR, Faustin Archange Touadéra pia amehutubu katika kikao hicho na kutoa wito kwa watu wa nchi yake kubadilisha mawazo na kupinga mauaji.

Askari wa kulinda amani nchini CAR

Jamhuri ya Afrika ya Kati ilitumbukia katika machafuko na mapigano mwaka 2013 wakati makundi ya Kikristo yanayobeba silaha yalipoanzisha mashambulio yaliyoratibiwa dhidi ya kundi la Seleka lenye Waislamu wengi zaidi, ambalo mnamo mwezi Machi mwaka huo liliiondoa madarakani serikali ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Francois Bozize. Hivi sasa kuna askari 10,000 wa kulinda amani katika nchi hiyo iliyo kati kati mwa bara la Afrika.