Ufaransa kushirikiana na nchi za Afrika katika mapambano dhidi ya ugaidi
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Bernard Cazeneuve amesema nchi yake itapanua ushirikiano wake na bara la Afrika katika kupambana na ugaidi.
Cazeneuve ameyasema hayo katika kikao cha pamoja na mawaziri wa mambo ya ndani wa nchi 11 za Kiafrika kilichofanyika mjini Paris na kusisitiza kwamba mapambano dhidi ya ugaidi kwa lengo la kugundua na kuzuia vitendo vya kufurutu mpaka yataendelea kwa msukumo mkubwa zaidi.
Mawaziri wa mambo ya ndani wa nchi za Afrika ikiwemo Benin, Cameroon, Ivory Coast, Guinea, Mali, Mauritania, Niger, Senegal, Chad na Togo walikutana na mwenzao wa Ufaransa jana Jumanne mjini Paris kujadili na kubadilishana mawazo kuhusu njia za kupambana na ugaidi na misimamo ya kufurutu mpaka.
Katika kikao chao hicho mawaziri hao walikubaliana juu ya utoaji mafunzo kwa askari polisi kwa ajili ya kupambana na misimamo ya kufurutu mpaka hasa miongoni mwa vijana na kuongeza operesheni za mazoezi ya kupambana na ugaidi.../