Askari 8 Misri wauawa katika mripuko wa bomu Peninsula ya Sinai
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i20119-askari_8_misri_wauawa_katika_mripuko_wa_bomu_peninsula_ya_sinai
Askari 8 wameuawa katika shambulio la bomu huko Sinai, kaskazini mwa nchi hiyo.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Nov 25, 2016 01:15 UTC
  • Askari 8 Misri wauawa katika mripuko wa bomu Peninsula ya Sinai

Askari 8 wameuawa katika shambulio la bomu huko Sinai, kaskazini mwa nchi hiyo.

Taarifa iliyotolewa na serikali ya Misri imesema kuwa, askari hao wameuawa katika shambulio la bomu la kutegwa ndani ya gari eneo la El-Arish katika mkoa wa Sinai, kaskazini mwa nchi hiyo.

Imeongeza kuwa, askari kadhaa pia wamejeruhiwa huku baadhi wakiwa mahututi. Tangu wiki kadhaa zilizopita, jeshi la Misri lilianzisha operesheni kubwa kwa ajili ya kuwafuatilia wanachama wa makundi yenye kufurutu ada na la kigaidi, ambapo katika operesheni hizo makumi ya wanamgambo waliokuwa na silaha wameuawa na wengine kujeruhiwa.

Magaidi wakiwa wakiendeleza harakati zao eneo la Sinai

Eneo la Peninsula ya Sinai limegeuka na kuwa uwanja wa harakati za makundi ya ukufurishaji, muhimu zaidi likiwa ni lile linalojiita la Answar Baitul-Muqaddas, ambalo baada ya kutangaza utiifu wake kwa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh, lilibadili jina lake na kuwa 'Wilaayat Sina.'

Kwa mara kadhaa kundi hilo limekuwa likitekeleza hujuma dhidi ya askari wa usalama wanaoenesha operesheni za kulisafisha eneo la Sinai tangu alipoondolewa madarakani rais wa zamani wa nchi hiyo, Muhammad Mursi hapo mwezi Julai mwaka 2013.

Wanazuoni wa Kisuni kabla ya kuchinjwa na magaidi wakufurishaji wa Kiwahabi eneo la Sinai

Miongoni mwa jinaiza hivi karibuni za magaidi hao wa Kiwahabi ni kuwaua kwa kuwachinja wanazuoni wawili wa Kisuni katika eneo hilo.