Ikhwani Misri yakanusha kuwa na uhusiano na makundi ya kigaidi
Nov 25, 2016 04:40 UTC
Harakati ya Ikhwanul Muslimina ya Misri imekanusha madai kuwa chama hicho kinashirikiana na makundi ya kigaidi.
Muhammad al Baltaji ambaye ni miongoni mwa viongozi wa harakati ya Ikhwanul Muslimina ya Misri amesema katika kikao cha kesi yake kuwa, harakati hiyo haina uhusiano wa aina yoyote na makundi yenye silaha na ya kigaidi japokuwa inahitilafiana na utawala wa sasa wa Misri.
Misri inaksumbuliwa na harakati za makundi yanayotumia silaha katika eneo la Sinai hususan lile linalojiita Ansaru Baitul Maqdis ambalo limetangaza utiifu wake kwa kundi la kigaidi la Daesh. Makundi hayo yamekuwa yakishambulia askari usalama na polisi ya Misri katika eneo hilo la Sinai.
Tags