Dec 10, 2016 03:05 UTC
  • Umoja wa Mataifa: Nchi za eneo la Pembe ya Afrika zipelekewe misaada

Umoja wa Mataifa umeitolea wito jamii ya kimataifa kutoa misaada zaidi kwa mamilioni ya watu katika eneo la Pembe ya Afrika wanaosumbuliwa na njaa.

Umoja wa Mataifa umesema katika ripoti yake ya mwezi Novemba kuwa, unaitolea wito jamii ya kimataifa kuwasaidia watu wa nchi za eneo la Pembe ya Afrika na kusisitiza kuwa raia wasiopungua milioni 29 katika eneo hilo wanahitaji msaada wa chakula.

Nchi za Pembe ya Afrika kama zilivyoonyeshwa katika ramani 

Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa imebainisha kuwa, kuna ongezeko la asilimia 18 ya watu wanaohitaji msaada wa chakula katika eneo la Pembe ya Afrika. Ripoti zinaonyesha kuwa, ukosefu wa chakula umeongezeka sana katika maeneo yaliyoathiriwa na migogoro kama Somalia, Sudan Kusini, Sudan na Burundi na vilevile katika maeneo mengine ambayo yamekuwa na mvua chache katika nchi za Pembe ya Afrika. 

Tags