Jan 09, 2017 07:17 UTC
  • Pua ya nguruwe na damu vyatapakazwa mbele ya msikiti Afrika Kusini

Baraza la Sharia la Waislamu wa Afrika Kusini (MJC) limelaani kitendo cha chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu kilichofanywa kwenye msikiti wa mji wa Simon katika jimbo la Cape Town cha kuweka pua ya nguruwe na kumwaga damu kwenye mlango wa msikiti huo.

Kiongozi wa MJC Maulana AK Allie amesema: "Baraza la Sharia la Waislamu linalaani ukiukaji wa heshima ya utu katika sura yoyote ile bila ya kujali dini ya mtu, na kuhusiana na hili ninaweza kusema kuwa kadhia hii inafanyiwa uchunguzi".

Amesema baraza hilo linalaani kitendo hicho na limetoa wito kwa Waislamu wa eneo hilo kukabiliana na kadhia hiyo kwa umaizi sambamba na kuheshimu sharia za nchi. Aidha amezitaka mamlaka za serikali kuwafatilia na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sharia waliohusika na kitendo hicho.

Waislamu wa Afrika Kusini katika hafla ya kidini

Habari ya tukio hilo la chuki dhidi ya Uislamu ambalo lilitokea siku ya Jumamosi baada ya Sala ya Alfajiri ilienezwa kupitia mitandao ya kijamii. Kwa mujibu wa baadhi ya mashuhuda, wakati polisi ya mji wa Simon ilipopewa taarifa ya tukio hilo ilieleza kwamba hakuna inachoweza kufanya na kwa hivyo haitofungua kesi kuhusiana na tukio hilo…/

 

Tags