CAR: Haki za watoto zinakiungwa sana
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i24193-car_haki_za_watoto_zinakiungwa_sana
Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati imeeleza wasiwasi wake mkubwa kutokana na hali mbaya ya watoto katika nchi hiyo iliyoathiriwa na vita vya ndani.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Jan 24, 2017 11:29 UTC
  • CAR: Haki za watoto zinakiungwa sana

Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati imeeleza wasiwasi wake mkubwa kutokana na hali mbaya ya watoto katika nchi hiyo iliyoathiriwa na vita vya ndani.

Waziri wa Masuala ya Jamii na Mapatano ya Kitaifa wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Virginie Mbaikoua amesema kuwa, haki za watoto zimekuwa zikivunjwa kwa kiwango kikubwa nchini humo tangu ulipoanza mgogoro wa ndani hapo mwaka 2013 na hali inakuwa mbaya siku baada ya siku licha ya hatua kadhaa zilizochukuliwa katika uwanja huo.

Image Caption

Waziri wa Masuala ya Jami wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amesema kuwa, masuala kama vile elimu, misaada kwa watoto walioathiriwa na ukatili wa kingono na kuzuia ndoa za utotoni yanapaswa kuwekwa katika orodha ya mambo yanayopaswa kupewa kipaumbele katika sera za serikali ya Bangui.

Jamhuri ya Afrika ya Kati ilitumbukia katika machafuko na mapigano ya ndani mwaka 2013 wakati makundi ya Kikristo yalipoanzisha mashambulio dhidi ya kundi la Seleka ambalo liliiondoa madarakani serikali ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Francois Bozize.