Misri yaanzisha mpango wa kuunda Jumuiya ya "Kaskazini mwa Afrika"
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i24629-misri_yaanzisha_mpango_wa_kuunda_jumuiya_ya_kaskazini_mwa_afrika
Misri imetaka ianzishwe "Jumuiya ya Kaskazini mwa Afrika".
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 03, 2017 04:10 UTC
  • Misri yaanzisha mpango wa kuunda Jumuiya ya

Misri imetaka ianzishwe "Jumuiya ya Kaskazini mwa Afrika".

Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Sameh Shokri ameandika kwenye ukurasa wake wa kijamii wa Twitter kuwa katika mazungumzo aliyofanya na mawaziri wa mambo ya nje wa Sudan, Algeria, Nigeria na Jamhuri ya Kongo pembeni ya kikao cha Umoja wa Afrika kilichofanyika nchini Ethiopia alipendekeza maudhui na mipango kadhaa ya pamoja ya kieneo ukiwemo wa kuunda Jumuiya yenye jina hilo, ya kaskazini mwa Afrika itakayoshirikisha nchi za Kiarabu na zisizo za Kiarabu.

Kikao cha AU kilichofanyika hivi karibuni Addis Ababa, Ethiopia

Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri aidha amesema, katika kikao hicho imeamuliwa pia kifanyike kikao cha mawaziri wa nchi za kaskazini mwa Afrika katika mji mkuu wa nchi hiyo Cairo haraka iwezekanavyo ili kuzungumzia suala hilo.

Ikumbukwe kuwa baada ya uhusiano wa Misri na Saudi Arabia kuvurugika kutokana na masuala ya kieneo ikiwemo kadhia ya mgogoro wa Syria, Cairo imeamua kutafuta washirika wengine badala ya Riyadh ili kuanzisha muungano na kushirikiana katika masuala mbalimbali…/