Al Nahdha: Tuko tayari kuipatanisha serikali ya Misri na Ikhwanul Muslimin
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i26318-al_nahdha_tuko_tayari_kuipatanisha_serikali_ya_misri_na_ikhwanul_muslimin
Mkuu wa harakati ya al Nahdha ya Tunisia amesema kuwa, harakati hiyo iko tayari kulipatanisha kundi la Ikhwanul Muslimin la Misri na serikali ya nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 13, 2017 03:27 UTC
  • Rached Ghannouchi, mkuu wa harakati ya al Nahdha nchini Tunisia
    Rached Ghannouchi, mkuu wa harakati ya al Nahdha nchini Tunisia

Mkuu wa harakati ya al Nahdha ya Tunisia amesema kuwa, harakati hiyo iko tayari kulipatanisha kundi la Ikhwanul Muslimin la Misri na serikali ya nchi hiyo.

Televisheni ya al Mayadeen imeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, Rached Ghannouchi, mkuu wa harakati ya al Nahdha ya Tunisia amesema kuwa, yuko tayari kutumia ushawishi wake kuipatanisha serikali ya Misri na Ikhwanul Muslimin ili kupunguza mivutano iliyopo baina ya pande hizo mbili.

Ameongeza kuwa, hadi hivi sasa hawajapata majibu yoyote ya pendekezo lao hilo na inaonekana mazingira hayaruhusu hivi sasa.

Wanachama wa Ikhwanul Muslimin wakiwa korokoroni Misri

 

Uhusiano baina ya serikali ya Misri na kundi la Ikhwanul Muslimin umeharibika mno tangu mwaka 2013 baada ya jeshi la nchi hiyo kumpindua Rais Muhammad Morsi kutoka Ikhwanul Muslimin

Hadi hivi sasa idadi kubwa ya wanachama na viongozi wa Ikhwanul Muslimin ya Misri wametekelezewa adhabu ya kifo au kuhukumiwa kifungo cha miaka mingi jela.